MIKE: THEA ANASUMBUA MOYO WANGU!

STAA wa filamu Bongo, Michael Sangu ‘Mike’ amefunguka ya moyoni kuwa mkewe waliyeachana naye, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ bado anausumbua moyo wake.

Akizungumza Mike alisema kuwa kamwe hawezi kuja kumsahau Thea kwani alikuwa akimpenda sana.
“Siwezi kuwa na mwanamke yeyote kwa sasa kwa sababu moyo wangu bado upo kwa Thea. Kiukweli anausumbua sana moyo wangu,” alisema Mike.
Wawili hao walioana miaka miwili iliyopita lakini walikuja kutengana kwa kile kilichoelezwa kukosa uaminifu kati yao.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini