IDADI YA WALIOKUFA MAAFA YA MAFURIKO KAHAMA YAFIKIA 47
IDADI ya watu waliofariki kutokana na mvua kubwa ya mawe, iliyopewa jina la tonado, sasa imefikia watu 47 baada ya majeruhi mwingine aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kufariki dunia juzi. Taarifa ya ongezeko la vifo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk Ally Rufunga alipokuwa akipokea misaada ya waathirika wa maafa hayo kutoka kwa watu mbalimbali, akiwemo Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe na mwakilishi wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa. Pia Rufunga alipokea misaada kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya ambaye alikabidhi vyakula na mafuta ya kula aina ya mawese lita 400, sabuni za kufulia katoni 32, chumvi kilo 357, dagaa gunia 12, mchele kilo 200 na maharage kilo 815. Vitu hivyo vilitolewa na wakazi wa mkoa wa Kigoma wa ajili ya kuwasaidia waathirika hao. Akikabidhi msaada kwa niaba ya familia ya Lowassa, Mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga, Khamis Mgeja alisema baada ya kutokea kwa maafa