Posts

Showing posts from February, 2015

Utafiti!! MAMBO 20 YANAYOFANYA NDOA IDUMU NA IWE YA FURAHA,TENDO LA NDOA LIMEKAMATA NAFASI YA 18!

Image
Kwa mujibu wa utafiti, tendo la ndoa sio siri ya ndoa yenye furaha. Siri ni mazungumzo ya uhakika.  Utafiti uliofanywa kwa wanawake na wanaume 2,000 waliooana kwa muongo mmoja au zaidi ushauri wao mkubwa kwa wanandoa wapya ni kuwa na desturi ya kuongea. Cha ajabu tendo la ndoa la kuridhisha lilikamata nafasi ya 18. Haya ni mambo 20 yaliyotajwa kwa umuhimu wake katika kuwa na ndoa itakayodumu na yenye furaha: 1. Ongeeni 2. Maridhiano/Kupatana 3. Endeleeni kusonga mbele 4. Ifanyie kazi 5. Usiikatie tamaa ndoa kirahisi 6. Msiende kitandani mkiwa mnabishana 7.Kuwa Mvumilivu 8. Sikiliza 9. Kuwa mkweli/muwazi 10. Kuwa na heshima 11. Kuwa Mvumilivu 12. Kuwa na matarajio yenye uhalisi 13. Usiolewe 14. Fanyeni vitu pamoja 15. Wasilianeni 16. Kuwa mstahimilivu 17. Kuwa mwaminifu 18. Kuwa na maisha yenye tendo la ndoa linaloridhisha 19. Kuweni marafiki 20. Jipeni nafasi Chanzo: Daily Mail

RADI YAUA MWALIMU NA WANAFUNZI 6 WAKIWA DARASANI

Image
Kamanda wa Polisi Mkoani kigoma, Jafari Mohamed. Wanafunzi sita, mwalimu wao, wamekufa papo hapo na wengine  11 kujeruhiwa kwa kupigwa na radi darasani wakati mvua kubwa zilizoambatana na kimbunga zikinyesha. Tukio hilo lilitokea  saa 2:30 asubuhi katika Shule ya Msingi Nyakasanda iliyopo kijiji cha Nyaphenda wilaya ya Kasuru mkoani Kigoma wakati mwalimu huyo na wanafunzi hao wakiwa darasani.   Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, John Ndunguru, alisema kuwa tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita wakati mvua hizo zikinyesha. Alisema mazishi ya mwalimu huyo na wanafunzi hao, yatafanyika leo mchana katika kijiji hicho chini ya usimamizi wa kamati ya ulinzi ya mkoa huo. Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.  Hata hivyo Mohamed,  alisema majina ya waliokufa yatafahamika leo wakati wa mazishi yao. Vilevile alisema wanafunzi wengine 10 na mwali...

Vifurushi vipya vya mitandao hasa MB 8: TCRA yatoa tamko na maagizo kwa makampuni ya simu

Image
Mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA imetoa tamko kuhusiana na malalamiko kutoka kwa watumiaji wa huduma za simu nchini kufuatia kubadilika kwa vifurushi vya mawasiliano.   Malalamiko hayo yalikuja baada ya baadhi ya mitandao ya simu kupunguza ukubwa wa data anazopata mtumiaji wa simu anapojiunga na vifurushi vya muda wa maongezi, sms na data kwa pamoja.   Baadhi ya mitandao imekuwa ikitoa Mega Bytes 8 peke yake ambazo kwa matumizi ya kawaida ni ndogo mno.   “TCRA imechambua mpangilio wa vifurushi – tozo za zamani na mpya na kugundua kwamba ingawaje baadhi ya watoa huduma wamebadilisha bei, kwa ujumla bei za muda wa kuzungumza na idadi ya meseji hazikubadilika sana.     "Hata hivyo, kuna upungufu mkubwa kwa idadi ya uniti za data (MBs),” amesema Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Jumanne.   Kupitia...

Joyce Kiria Adaiwa Milioni 500 kama Fidia ya Kumdhalilisha Mbunge Kupitia Kipindi cha Wanawake Live

Image
Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria amepokea samansi ya mashtaka kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir (CCM) ambaye amedai amlipe fidia ya kumdhalilisha sh. Milioni 500 au amuombe radhi kupitia  kipindi chake. Akiongea na Mwandishi wetu, Joyce Kiria alisema kuwa amepokea barua hiyo kwa mikono miwili na anawasubiri wanasheria wake ili waijadili. “Nilimpokea mke wa Mbunge aitwaye Hawa kama mwanamke mwenye matatizo ambaye alifika kutoa sauti yake ili watu wamsaidie mtoto wake mwenye ulemavu.   "Baada ya kuongea naye nilimtafuta mheshimiwa ili kumpa nafasi naye aongee ya kwake kama wajibu wangu, lakini cha kushangaza yeye alinikamata na kunipeleka polisi, leo anasema nimemdhalilisha,” alisema Joyce .   Joyce anadaiwa fidia na Mbunge huyo kwa kuitangaza habari ya kumtelekeza mtoto mlemavu ambaye alipelekwa kwenye kipindi chake na mkewe, Hawa Deusi.   

Picha za Mzishi ya Msanii Mez B Yaliyofanyika Mkoani Dodoma

Image
MAMIA ya mashabiki na wasanii wa muziki wa kizazi kipya, juzi walijitokeza kuupumzisha mwili wa msanii, Moses Bushangama ‘Mez B’, katika makaburi ya Wahanga wa Treni, Mailimbili mkoani Dodoma.   Akizungumza wakati wa kuuaga mwili huo, mama wa marehemu, Mchungaji Mary Katambi, aliwataka vijana kumrudia Mungu.    “Mwanangu aliuona uwepo wa Mungu, nilikuwa nikimsihi kuokoka na kumrudia Mungu na alikuwa akinijibu itafika wakati mimi wa yeye kufanya hivyo,” alisema Mary.    Upande wake msanii wa kundi la Chemba Squad, Noorah alisema wamesikitika kumpoteza Mez B kwani alikuwa ni msanii anayependa ushirikiano na pengo lake halitaweza kuzibika. Wananchi wakiwa wamebeba  mwili wa marehemu Marehemu Mez B baada ya kuagwa na mashabiki wa mziki pamoja na ndugu jamaa na marafiki mwili wake ulielekea kupumzishwa katika makaburi ya Wahanga Maili mbili juzi. Mama mzazi wa Mez B, Marry Mkandawile (katikati) akiwa ameshi...

CHADEMA WADAI KUENDELEA KUZUNGUMZIA KASORO ZA UANDIKISHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA PG4A2718

Image
Chama cha demokrasia na Maendeleo chadema kimesema kuwa licha ya kuendelea kuwaelimisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, chama hicho pia hakitasita kuzungumzia changamoto zinazojitokeza wakati wa zoezi hilo Kauli hiyo imetolewa na naibu katibu mkuu wa chama hicho Bara Mh. John Mnyika mara baada ya ufunguzi wa zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura lililofanyika kitaifa makambako mkoani Njombe Mnyika amesema wanaipokeaa kwa mikono miwili kauli ya mwenyekiti wa Tume ya taifa ya uchaguzi kuwa vyama viwahamasishe wananchi kujiandikisha, na wao watazidi kufanya hivyo kwa kadri ya uwezo wao. Wakati huo huo Mwenyekiti wa tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC) jaji mstaafu Damian Lubuva amesema teknolojia mpya ya kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura ni kwa ajili ya uandikishaji tu na halitatumika katika upigaji kura wala kuhesabu Akizungumza wakati wa uzinduzi wa uboreshaji wa daftari hilo la wapiga...

Vurugu Ilula Mkoani Iringa, Mwananchi afariki, Kituo cha Polisi chachomwa moto!

Image
  WANANCHI wenye hasira mjini Ilula, mkoani Iringa, Jana wamevamia kituo cha polisi na kuvunja milango kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma moto baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili. Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, tukio hilo limetokea jana asubuhi kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina lake kujigonga ukutani na kuanguka kisha kufariki dunia wakati akiwakimbia polisi waliokuwa kwenye oparesheni ya kuwakamata watu wanaokunywa pombe wakati wa asubuhi. Habari zaidi zinapasha kwamba, licha ya kuchoma moto magari, waliziba barabara kuu ya kwenda mikoani na kuyazuia magari kupita, hali iliyosababisha polisi kuwakabili lakini walizidiwa nguvu na kuingia ndani ya basi la UPENDO. Askari wakiwa ndani ya gari hilo waliendelea kushambuliwa na wananchi kwa mawe na kuvunja vioo vyake.

KESI YA DAWA ZA KULEVYA ZA MABILIONI ZAWAFIKISHA MAHAKAMANI WATU HAWA HAPA

Image
WATU watano akiwemo raia wa Uingereza wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashitaka ya kukutwa wakisafirisha gramu 2870.781.36 za dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni tano. Washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka manne mbele ya Mahakimu wawili tofauti. Washitakiwa hao ni raia wa Uingereza Halid Mahunga, wafanyabiashara Anna Mboya, Fred William, Kambi Zuberi na Hamis Mtou (32), wakazi wa Dar es Salaam.   Katika mashitaka yanayomkabili Mboya, Wakili wa Serikali Mwandamizi Evetha Mushi alidai mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa kuwa Januari 2, mwaka 2011 Mboya akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere alikutwa akiingiza nchini gramu 1195.45 dawa za kulevya aina ya cocaine zenye thamani ya Sh 46,296,200. Washitakiwa wengine William na Zuberi walifikishwa mbele ya Hakimu Riwa na kusomewa mashitaka ya kuingiza nchini dawa hizo zenye thamani ...

ELIMU YA MSAADA WA KISHERIA YAENDELEA KUWAOKOA WANANCHI WA KATA YA LUPILA MAKETE

Image
 Na eddyblog, Makete Wananchi wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kujitokeza kupatiwa msaada wa kisheria, na wasaidizi wa kisheria waliopo wilayani hapo ili kuwasaidia kutatua migogoro mbalimbali inayowakumba kutokana na ukosefu wa elimu ya sheria Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa chama cha wasaidizi wa kisheria wilayani Makete PACEMA ambaye pia ni msaidizi wa kisheria kata ya Lupila Bw. Nebert Sigala wakati akizungumza na mwandishi wetu kuhusu elimu ya masuala ya kisheria katika kata hiyo Bw. Sigala amesema kwa hivi sasa wapo wananchi ambao wamekuwa wakijitokeza kupatiwa msaada wa kisheria ambao umekuwa ukiwasaidia katika matatizo yaliyokuwa yakiwakabili kwa kuwa hawakuwa na uelewa huo toka awali Ametaja baadhi ya maeneo ambayo yamekuwa yakihitajika zaidi na wananchi hao kuwa ni sheria za ardhi, sheria ya mtoto pamoja na sheria mbalimbali za nchi, jambo ambalo limewasaidia wananchi wa kata hiyo kuona umuhimu wa kumiliki ardhi kisheria

TAARIFA HII MPYA KUTOKA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Image

UGANDA YAAIBIKA KWA PICHA HIZI ZA MSANII HUYU MAARUFU NCHINI HUMO

Image
Picha  chafu  za  Msanii  maarufu  wa  kike  nchini  Uganda  zimevuja  na  kusambaa  kwa  kasi  mtandaoni..... Picha  hizo  Ambazo  zilianza  kusambaa  jana  zinamuonyesha  msanii  huyo  akiwa  kitandani  na  njemba  moja  huku  akiwa  mtupu  kama  alivyozaliwa..... Picha  nyingine  zinamuanika  akiwa  mtu  na  wasichana  wenzie  kitandani..... ZIANGALIE KWA KUBONYEZA NENO IMAGE Image1 Image2 Image3 Image4 Image5 

WARSHA KUHUSU NAFASI YA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUZUIA UKATILI DHIDI YA WATOTO NCHINI TANZANIA YAFUNGULIWA KILIMANJARO

Image
 Baadhi ya washiriki wa Warsha wakifuatilia kwa makini  Mmoja wa  washiriki wakiuliza maswali katika warsha hiyo. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa ushirikiano na UNICEF wameandaa warsha ya siku tatu inayohusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuzuia ukatili dhidi ya watoto nchini Tanzania. Warsha hiyo inayofanyika mjini Moshi inashirikisha wawakilishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Wawakilishi kutoka Mkoa wa Kilimanjaro, Wawakilishi kutoka wilaya za Hai na Moshi Manispaa, wawakilishi kutoka UNICEF pamoja na wawakilishi wa redio 14 zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto. Wengine ni wawakilishi kutoka Baraza la Habari Tanzania, mwakilishi kutoka Csema pamoja na waandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto kampuni ya True Vision Production. Akifungua warsha hiyo, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Kilimanjaro, Paul Shayo alilishukuru shirika la Watoto Duniani (UNICEF) kwa kazi nzuri ambazo wamekuwa wakizifanya ...