Flora Mbasha Afunguka Mazito Mpaka Mengine Hayawezi Elezeka Kuhusu Mumewe Mbasha, Ni Hatari Sana

Nimefikia uamuzi wa kudai talaka kutokana na kuchoshwa na vitendo vya ukatili nilivyokuwa nafanyiwa na mume wangu, kwa zaidi ya miaka 8 na hata sasa bado anaendeleaje, Kwani hata kuongea uongo kwenye media juu yangu ni ukatili pia.. nimekuwa nikinyanyaswa kijinsia na Mume wangu na sikuwahi kutoa taarifa mahala popote kutokana na vitisho alivyokuwa akinitisha.
Watu Wengi wanafikiri nilikuwa na ndoa nzuri sana lakini kumbe nilikuwa Nikivumilia tu Kwani niliamini ipo siku atabadilika maana nilimpenda sana mume wangu.Nilijaribu kuficha huzuni na maumivu yangu kila nilipotoka na mume wangu kwenda kwenye Huduma au mahala pengine penye mkusanyiko wa watu.

Sijawahi hata Mara moja kutoa taarifa hata kwa wazazi wangu juu ukatili niliokuwa nafanyiwa na mume wangu.Kwanza sikutaka kumvunjia heshima kwa ndugu zangu na pia alikuwa akinitishia kuniua na kuongeza kunifanyia ukatili huo.
Kutokana na historia yake ya nyuma alikuwa na uwezo wa kunifanya chochote na ndiyo maana nilikuwa nikimwogopa sana.
Siku zote nilikuwa akilala na panga kitandani ambalo ndilo alikuwa akinipiga nalo na kuapa kunichana chana Mwili Kabla ya kuniua.
Kipigo hicho nimekuwa nikikipata hata ninapokuwa kwenye Huduma bila kujali natakiwa kuwa kwenye mood nzuri ili ni perfome vizuri.
Nimevumilia muda mrefu lakini ndo mateso yakawa yanazidi na kufikia hatua ya kufukuzwa akidai yeye ana mwanamke mwingine wa dini yake ya zamani hivyo anataka amlete hapo nyumbani.
Nilikataa kuondoka na kumwambia amlete tu, tutaishi wote mimi nitakuwa nikilala chini maana nshazoea siku zote Amekuwa akinilaza chini ,alivyoona siku zinazidi kwenda na mimi nimegoma kuondoka basi akaamua sasa isiwe siri ya chumbani tena Akawa ananitoa ananipigia sebuleni na anasema nataka mtoto na wengine wote wajue kuwa huwa nakupiga humu ndani.Ikafika hatua anataka kunitoa nje ya geti ili majirani wajue kuwa huwa napigwa na anifukuze mbele yao.
Kwa Miaka yote alinizuia kufungua account bank na kudai kuwa yeye ndo mwanaume hivyo pesa zote ataweka yeye. So pesa zangu zote nilizokuwa naingiza alikuwa akichukuwa yeye na kuzihifadhi kwa account yake binafsi.
Sikuwa nikibaki hata na mia.Nilijaribu kufanya biashara lakini napo pesa zote akawa akichukuwa yeye ikabidi niache.. Nikitaka hata vocha ya mia tano Lazima nimwombe hela na niitolee maelezo ninampigia nani.
Mume wangu kwa kipindi chote hakuwahi kuwa na kazi yoyote zaidi ya kunifanya mimi ndo biashara yake. Lengo lake ilikuwa ni kunitumia mimi kwa maslahi yake na sio upendo kama mke wake.
Hakuwahi kunipenda hata yeye mwenyewe hukiri kuwa alinioa tu basi ili afanikiwe kwenda ulaya kwa kuwa mimi nilikuwa nikisafiri na babu yangu.
Na yeye kila akijaribu kwenda nje anashindwa. Kuna mambo mengi ya ukatili aliyokuwa akiyafanya ndani siwezi kuyasema kwa ajili ya maadili na pia bado Ninamheshimu kama mzazi mwenzangu. Alipoona siondoki pamoja na vipigo, matusi na kunifukuza kote.
Akasema nitahakikisha nakufanyia jambo ambalo utaondoka mwenyewe humu ndani bila kupenda sitaki kuzungumzia suala ambalo liko mahakani ingawa hilo nahisindilo alilokuwa kadhamiria ili tu niondoke.
Nilijaribu sana kumsihi tukae kikao na wazee ili watushauri na kutusaidia lakini nilikuwa nikiambulia matusi tu ya nguoni ambayo siwezi kuyaandika hapa.
Siku niliyoondoka nyumbani alidhamiria kuniua alidai hata akiniuà hakuna atakaye amini kuwa ni yeye kaniua, na ni kweli maana sikuwahi kushtaki mahala popote.
Alichukuwa panga akanipiga nalo kisha akaniniga hadi nikaishiwa nguvu .Aliponiachia sielewi nilitokaje ndani. Ugomvi mkubwa ulitokana na mimi kukataa kufanya tenda la ndoa kinyume na maumbile.
Amekuwa Alinipiga na kunilazimisha kufanya tenda hilo kinyume na maumbike kwa miaka mingi lakini nikisema bora nife kuliko kutendewa ukatili huo.Amekuwa akidai kuwa wanawake tumeumbwa ili tufanyiwe tenda hilo la ndoa mbele na nyuma so ni haki yake.
Niliondoka kwake nikiwa na sh elfu mbili tu. Nilimwachia kila kitu nyumba gari na pesa zote zikiwa kwa account yake zaidi ya milioni 50.Sikuwa na uwezo wa kutoa pesa maana ni account yake binafsi.
Nimejitahidi sana kumwita kwenye vikao hata vya familia ili tu tujaribu kuzungum za lakini amekuwa akionesha dharau tu na kusema yeye haitaji ndoa tena anaoa mke mwingine hivyo hawezi kusuluhishwa.
Ingawa Amekuwa akidanganya sana kwenye media. Nilimwuliza Unapata faida gani unapodanganya watu kuhusu mimi?
Akasema yeye amechafuka kwa ubakaji so acha na mimi nichafuke na akasema atahakikisha sifanyi huduma sehemu yoyote labda nihame nchi.
Kama msg hizo angekuwa amezituma bila kuandika na matusi ningezikopi but zaidi kauli zake ni za matusi. Hivyo imefika mahali nimeona bora tuachane kisheria na pia nipate haki yangu maana mume wangu anajivunia mali ambazo hakuzitolea jasho yeye na huku anawatapeli watu kwa kudai kuwa hana pesa maana mimi nimeondoka nazo wakati ni uongo mtupu.
Mimi ninapanda daladala siku hizi sababu sina uwezo wa kuwa na gari hadi niazime kwa marafiki zangu. Mume wangu amekataa hata kumsomesha mtoto sasa hivi nahangaika kutafuta ada ili mtoto arudi shule lakini pesa yote anayo anayo Mbasha.
Sasa sijui hapo ananikomesha mimi au mwanaye.!maana urithi wa mtoto ni elimu bora na mzazi anayempenda mwanaye atapambana ili kuhakikisha mtoto anapata elimu bora.
Nilikaa kimya muda mrefu sikutaka kuzungumza lakini imefika mahali Nimechoka maana huyu bwana hajiheshimu. Tukikutana anasema sio yeye anayepeleka habari mitandaoni.
Ninaomba wanaume wenyewe Mfano wake waache kuwafanyia ukatili wake zao majumbani.Najua wako Wengi sana wanao nyanyasika kama ilivyo kuwa kwangu lakini Hawana sehemu za kukimbilia Hivyo wanavumilia tu na mwisho wa siku wanakufa na kuacha watoto wakiteseka.
Mimi Nilivumilia zaidi ya Miaka 8 lakini imefika mahali enough is enough. Maandiko matakatifu yanasema, ndoa haivunjwi isipokuwa kwa uasherati.
Acha nife kwa mapenzi ya Mungu na sio kwa mapenzi ya mtu..Na ni naamini sitakufa mpaka ndoto zangu zitimie.
Mume wangu ameapa kuwa atahakikisha sifanyi Huduma tena lakini ninasema katika Jina la YESU, kama Bwana aishivyo, mwanzilishi wa huduma yangu ni Mungu Hivyo mmalizaji wa Huduma yangu ni Mungu mwenyewe.
Na sasa ninajipanga kumwimbia Mungu kama sitaimba tena.Wakati mwingine usipokuwa mwangalifu ndoa inaweza kukukosesha ufalme wa mbinguni hasa Ukiingia kwenye ndoa isiyo sahihi. Ninampenda sana mume wangu lakini ninampenda Mungu wangu zaidi. Ahsante.
Nimeamua kuandika Maana Nimechoka kuficha maovu aliyokuwa akinitendea.Nimemtunzia heshima muda wote maana sikutaka jamii imjue ni mtu wa aina gani but yeye anatumia ukimya wangu kama udhaifu so naona bora niweze wazi ili jamii imtambue mimi yamenikuta najua Wapo Wengi tu wanapitia mateso niliyoyapitia mimi.
Kutokana na vitisho wanaendelea kunyanyaswa. That is not honest kwa kweli.Mimi ningekufa Kabla ya wakati wangu lakini namshukuru Mungu niko hao hata sasa na pia ili kuwaonya wanaume wanaume wenyewe tabia kama yake.
Kama umemshoka mwanamke achaneni kwa amani sio kumnyanyasa mwanamke kama alivyokuwa anafanya Mbasha kwangu.
Ninapinga vikali unyanyasaji wa wanawake na watoto majumbani.





Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini