ELIMU YA MSAADA WA KISHERIA YAENDELEA KUWAOKOA WANANCHI WA KATA YA LUPILA MAKETE
Na eddyblog, Makete
Wananchi
wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kujitokeza kupatiwa msaada wa
kisheria, na wasaidizi wa kisheria waliopo wilayani hapo ili kuwasaidia
kutatua migogoro mbalimbali inayowakumba kutokana na ukosefu wa elimu ya
sheriaRai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa chama cha wasaidizi wa kisheria wilayani Makete PACEMA ambaye pia ni msaidizi wa kisheria kata ya Lupila Bw. Nebert Sigala wakati akizungumza na mwandishi wetu kuhusu elimu ya masuala ya kisheria katika kata hiyo
Bw. Sigala amesema kwa hivi sasa wapo wananchi ambao wamekuwa wakijitokeza kupatiwa msaada wa kisheria ambao umekuwa ukiwasaidia katika matatizo yaliyokuwa yakiwakabili kwa kuwa hawakuwa na uelewa huo toka awali
Ametaja baadhi ya maeneo ambayo yamekuwa yakihitajika zaidi na wananchi hao kuwa ni sheria za ardhi, sheria ya mtoto pamoja na sheria mbalimbali za nchi, jambo ambalo limewasaidia wananchi wa kata hiyo kuona umuhimu wa kumiliki ardhi kisheria