ASKARI WA JWTZ AUAWA KINYAMA, VIUNGO VYA MWILI WAKE VYANYOFOLEWA IKIWEMO SEHEMU ZA SIRI

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kikosi cha 27 Makoko kilichopo Musoma, Praiveti Wilfred Koko amekutwa ameuawa na kuondolewa sehemu ya viungo vya mwili katika eneo la kikosi hicho.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mkoani Mara ilisema askari huyo MT-78227, aliokotwa katika eneo la jeshi Januari 30, mwaka huu saa sita mchana mwili wake ukiwa hauna baadhi ya viungo ukiwemo mguu wa kulia, viganja vya mikono yote na sehemu za siri.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ernest Kimola, alisema upande wa mguu wa kushoto wa marehemu ulikutwa na jeraha lililokatwa na kitu chenye ncha kali hali inayoonyesha huenda askari huyo aliuawa na kutupwa kwenye eneo hilo.
Alisema huenda viungo vya askari huyo ambavyo havikukutwa vilikuwa vimeliwa na wanyama baada ya mwili huo kuonekana kukaa muda mrefu, kuanza kuharibika na kuingiliwa na wadudu.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini