WARSHA KUHUSU NAFASI YA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUZUIA UKATILI DHIDI YA WATOTO NCHINI TANZANIA YAFUNGULIWA KILIMANJARO

 Baadhi ya washiriki wa Warsha wakifuatilia kwa makini
 Mmoja wa  washiriki wakiuliza maswali katika warsha hiyo.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa ushirikiano na UNICEF wameandaa warsha ya siku tatu inayohusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuzuia ukatili dhidi ya watoto nchini Tanzania.

Warsha hiyo inayofanyika mjini Moshi inashirikisha wawakilishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Wawakilishi kutoka Mkoa wa Kilimanjaro, Wawakilishi kutoka wilaya za Hai na Moshi Manispaa, wawakilishi kutoka UNICEF pamoja na wawakilishi wa redio 14 zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.

Wengine ni wawakilishi kutoka Baraza la Habari Tanzania, mwakilishi kutoka Csema pamoja na waandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto kampuni ya True Vision Production.

Akifungua warsha hiyo, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Kilimanjaro, Paul Shayo alilishukuru shirika la Watoto Duniani (UNICEF) kwa kazi nzuri ambazo wamekuwa wakizifanya kwa kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa Haki za Watoto zinatekelezwa hapa nchini. 


Paul alitaja aina za ukiukwaji wa haki za mtoto hapa nchini kuwa ni pamoja na kuolewa katika umri mdogo, kutumikishwa katika mashamba na ukatili dhidi ya watoto. Hata hivyo aliendelea kuzitaja athari mbalimbali zinazotokana na ukiukwaji wa haki hizo kuwa ni pamoja na watoto kukatishwa masomo na kukosa haki ya kuendelezwa na kwamba ndoa za utotoni zina madhara kiafya hasa wana

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini