Picha za Mzishi ya Msanii Mez B Yaliyofanyika Mkoani Dodoma

MAMIA ya mashabiki na wasanii wa muziki wa kizazi kipya, juzi walijitokeza kuupumzisha mwili wa msanii, Moses Bushangama ‘Mez B’, katika makaburi ya Wahanga wa Treni, Mailimbili mkoani Dodoma.
 
Akizungumza wakati wa kuuaga mwili huo, mama wa marehemu, Mchungaji Mary Katambi, aliwataka vijana kumrudia Mungu. 
 
“Mwanangu aliuona uwepo wa Mungu, nilikuwa nikimsihi kuokoka na kumrudia Mungu na alikuwa akinijibu itafika wakati mimi wa yeye kufanya hivyo,” alisema Mary.
 
 Upande wake msanii wa kundi la Chemba Squad, Noorah alisema wamesikitika kumpoteza Mez B kwani alikuwa ni msanii anayependa ushirikiano na pengo lake halitaweza kuzibika.
IMG-20150223-WA0040
Wananchi wakiwa wamebeba  mwili wa marehemu Marehemu Mez B baada ya kuagwa na mashabiki wa mziki pamoja na ndugu jamaa na marafiki mwili wake ulielekea kupumzishwa katika makaburi ya Wahanga Maili mbili juzi.
IMG-20150223-WA0036
Mama mzazi wa Mez B, Marry Mkandawile (katikati) akiwa ameshikiliwa na ndugu baada ya kuingia viwanja vya Mashujaa ili kutoa heshima za mwisho.
IMG-20150223-WA0037 IMG-20150223-WA0038
Baadhi ya wasanii waliohudhuria msiba wa Mez B wakiwa kwenye majonzi mazito
IMG-20150223-WA0039  IMG-20150223-WA0041 IMG-20150223-WA0042 IMG-20150223-WA0044
Mtangazi wa Citizen TV anayejulikana kwa jina la Mzazi Willy Tuva akifanya mahojiano na msanii wa Bongo Fleva Janjaro.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini