DIAMOND: BORA NIFE KULIKO KUMRUDIA WEMA
Musa mateja KIAPO! Kuonesha kwamba hana mpango wa kurudi nyuma, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ amefungukia msimamo wake juu ya mwandani wake wa zamani, Wema Sepetu ‘Madam’ kwa kusema kuwa kamwe hawezi kumrudia tena, Risasi Jumamosi lina mkanda kamili. Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’. Licha ya Diamond kufunguka hayo, wawili hao wamekuwa na mapenzi ya vipindi, kuna wakati waliwahi kumwagana kisha kurudiana na hakuna aliyewahi kutoa tamko zito lakini safari hii Diamond amesema ndiyo basi tena! TUJIUNGE NA CHANZO Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na staa huyo, mara kwa mara Diamond amekuwa akijiwekea nadhiri ndani ya moyo wake na kusisitiza kwamba pamoja na kuwa maisha ya sasa huendeshwa kwa msingi wa fedha lakini hata kama ‘atafulia’ kiasi gani, ni bora afe maskini kuliko kurudiana na Wema. “Diamond amekuwa akisema kila wakati kwa msisitizo kuwa kutokana na matatizo aliyokumbana nayo katika uhusiano wake kwa...