Jeshi la polisi jijini Tanga lasambaza askari wake kuimarisha ulinzi katika kipindi hiki cha sikukuu
Jeshi
la polisi mkoani Tanga limesambaza askari katika makanisa yote jijini
Tanga kufuatia hivi karibuni kuibuka kwa viashiria vya ugaidi
vilivyosababisha waumini wa madhehebu mbali mbali kuwa na hofu kwenda
katika mkesha wa sikukuu ya pasaka.
Akizunguza
jijini Tanga kuhusu jitihada za jeshi katika kuimarisha ulinzi na
usalama katika nyumba za ibada kuanzia jana kwenye ibada za ijumaa kuu
hadi jumatatu ya pasaka,kaimu kamanda wa polisi mkoani tanga Bwana Juma
Ndaki amewataka waumini wasiwe na hofu hata kama wakiona idadi kubwa ya
askari katika nyumba za ibada kwa sababu ni sehemu ya utekelezaji katika
zoezi la kuimarisha ulinzi na usalama.
Katika
hatua nyingine mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Daleda Masaka
amekufa baada kuanguka katika mapango ya amboni wakati alipokuwa
akivunja mawe kwa ajili ya kupata kokoto ndipo alipokanyaga jiwe kubwa
lililokuwa limejiegesha katika shimo ambalo hutumika kuweka baruti kwa
ajili ya kulipua mawe kisha kutumbukia na kufunikwa na jiwe hilo.
Kufuatia
hatua hiyo mratibu wa makundi yanayojihusiha na kuponda mawe kwa ajili
ya kutengeneza kokoto amewaagiza wadau wa kazi za kuvunja mawe kuacha
zoezi hilo mara moja kufuatia mvua zinazoendelea kunyeesha kuharibu
sehemu ya mawe na kusababisha kuteleza na kuanguka kutoka milimani hatua
ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa zaidi ya hayo.