"MCHAWI" APIGWA NA KUTELEKEZWA AKIWA NA MAJERAHA YAKE HUKO GEITA


Mwanamke mmoja aliyejeruhiwa na wananchi ametelekezwa barabarani na wauguzi wa Zahanati ya Nzera iliyopo Geita kwa kile kinachodaiwa ni mchawi.
Hata hivyo kaimu mganga wa Zahanati hiyo Bigaeli Kasala alipinga madai hayo akisema hajatelekezwa bali bali alikuwa akitafutiwa usafiri wa kumpeleka Geita kwa matibabu zaidi.
“Huyu mgonjwa hatujamtupa,niliwakabidhi wahusumu wampandishe basi la asubuhi linalokwenda Geita lakini inaonekana walipitwa na basi hivyo wakamuacha barabarani akisubiri basi jingine”-Kasala.
Dk. Kasala alisema kituo chao hakina gari la wagonjwa ndio maana walimwacha barabarani akisubiri gari lingine.
Awali alidai mwanamke huyo alipelekwa Zahanati hapo wa kituo ch polisi baada ya kumwokoa mikononi mwa wananchi waliokuwa wakimpiga wakimtuhumu kuwa ni mchawi.
Alisema alikutwa kwenye nyumba akiwa mtupu na kutuhumiwa alikuwa akifanya uchawi na ndipo watu wakaanza kumpiga hadi kumvunja kiuno.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini