Taarifa kuhusu upotoshaji wa mswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015

 Taarifa kwa vyombo vya Habari , 4 Aprili 2015
Taarifa kuhusu upotoshaji wa mswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015

Naomba nifafanue kuhusu propaganda inayoenezwa na maafisa wa TCRA kupitia CloundsFM kuhusu Sikika na Mswada wa ‪#‎CyberCrimeBill‬.

Sikika haikuhudhuria mkutano wa wadau unaodaiwa kufanyika Dodoma kama ilivyodaiwa na Mh Peter Serukamba na leo maafisa wa TCRA.

Sikika haikutoa maoni kuhusu Mswada wa miamala ya kielektoniki kama ilivyodaiwa na Mh Peter Serukamba na pia leo maafisa wa TCRA.

Sikika ilituma maoni ya pamoja ya wadau kwa niaba ya wadau kuhusu #CyberCrimeBill kwa njia ya email kwa Mkiti Kamati Mh Peter Serukamba.

Maoni hayo hayakutumika kuboresha #CyberCrimeBill bali kuongeza tu orodha ya wadau wanaoda iwa "kushiriki" kwa lengo la kuonesha kuridhia.

Kwa kuwa maoni ya wadau hayakuzingatiwa na kwamba ‪#‎CiberCrimeBill‬ iliyopitishwa ina mapungufu mengi, Sikika na wadau bado wanaipinga.

Mwisho tunaomba jina la Sikika lisiendelee kutumika kuhalalisha upitishwaji wa sheria hii.

Irene Kiria
Mkurugenzi wa Sikika
4 Aprili 2015.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini