WATU WAANZA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA JIMBO LA MBINGA MAGHARIBI LILILOACHWA WAZI NA KEPTENI KOMBA


Marehemu John Komba enzi za uhai wake...

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Taasisi ya Taaluma na Maendeleo, Dk. Stephen Maluka, ametangaza nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la Nyasa (Mbinga Magharibi) mkoani Ruvuma kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Oktoba mwaka huu.
Dk. Maluka mwenye Shahada ya Uzamivu ya Afya ya Jamii aliyopata nchini Sweden, amejitosa kugombea jimbo hilo ambalo awali lilijulikana kama Mbinga Magharibi na lilikuwa likiongozwa na marehemu Kapteni John Komba ambaye alifariki mwanzoni mwa mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana Dk. Maluka alisema lengo la kuingia katika kinyang’anyiro hicho ni kuwakomboa wananchi wa jimbo hilo, ambao kwa sasa  wana hali ngumu ambayo ilichangiwa na  usimamizi mbovu wa rasilimali na bajeti za Serikali.
Alisema upungufu uliopo katika jimbo hilo ni wa kiuongozi na endapo kutatokea mtu atakayekuwa na usimamizi mzuri katika masuala muhimu atakuwa na nafasi nzuri ya kubadilisha maisha ya wananchi waliopo.
“Nalijua Jimbo la Nyasa matatizo yote yanatokana na usimamizi mbovu wa viongozi katika miradi ya Serikali na fedha za bajeti zinazotolewa kwa ajili ya jimbo hilo.
Alisema endapo atapata nafasi hiyo atasimamia kwa umakini mapato na matumizi ya jimbo ili kuhakikisha yanamnufaisha kila mwananchi.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini