NEC yaongeza muda wa kujiandikisha Makambako mkoani Njombe

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeongeza muda wa siku mbili zaidi katika zoezi la uandikishaji wapiga kura kwenye daftari lakudumu la wapiga kura kwa njia ya Biometric voters registration (BVR) lililokuwa limalizike hii leo katika halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kujiandikisha.
 
blog hii  ilifika katika baadhi ya vituo kwenye mitaa ya mji wa Makambako na kukuta misururu ya watu walio na shauku ya kujiandikisha katika daftari hilo ili kuwahi muda wa kufunga zoezi hilo huku baadhi yao wakieleza kuwa muda wa wiki moja kufanya zoezi hilo uliopangwa na tume ya taifa ya uchaguzi hautoshi kwani watu wengi hawajajiandikisha bado hadi leo.
 
Majira ya saa kumi jioni tulifika katika ofisi za halmashauri ya mji wa Makambako na kuzungumza na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bibi Vumilia Nyamoga ambaye ameeleza namna zoezi linavyoendelea na kutoa tangazo hilo la tume ya uchaguzi linaloeleza kuongezwa muda wa zoezi hilo na sababu za uamuzi huo.
 
Aidha afisa huyo mwandikishaji Bibi Nyamoga ameeleza kuwa kutokana na mwitikio huo wa watu kujitokeza kujiandikisha wameweza kuvuka lengo la kuandikisha watu elfu 33 lililowekwa na tume ya taifa ya uchaguzi hapo awali huku watu wakiendelea kumiminika kutaka kujiandikisha katika daftari hilo lakudumu.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini