Posts

Showing posts from 2014

SHEIKH SHARIF AZUA MAPYA YA URAIS 2015, SOMA UONE

Image
Sheikh Shariff Matongo  akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake  jijini Dar es Salaam (hawapo pichani)kuhusu  ndoto yake ambayo ameoteshwa kuelekea mwaka 2015. NA CHALILA KIBUDA,GLOBU YA JAMII,DAR. Sheikh Sharif Matongo amesema ameoteshwa ndoto ya mwaka 2015 na kupata ushauri kwa mashekh mbalimbali Duniani ambavyo vitatokea nchini na viongozi wasipuuze ndoto hiyo. Sharif aliyasema hayo leo ofisini kwake alipokutana na waandishi wa habari ,alisema ameoteshwa mambo saba likiwemo la kupata Rais ajaye ambaye kiongozi ambaye muda mwingi ameishi nje ya nchi kwa kufanya kazi. Alisema katika ndoto nyingine kifo cha kiongozi mkubwa  ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali na  mwenye kambi katika Chama cha Mapinduzi (CCM).  Sheikh  alisema ndoto nyingine  kutokea kwa mvua nyingi ambapo watu wanaoishi mabondeni ,kutokea kwa vifo vya watoto vingi ,wafanyabiashara kupata mafanikio  makubwa kwa mwaka utaoanza kesho. Vijana wengi watash

inasikitisha saana..HALI MBAYA YA HEWA YAKWAMISHA ZOEZI LA UOKOAJI MIILI KUTOKA AIRASIA QZ8501

Image
Baadhi ya mabaki ya Ndege ya AirAsia yakiwa Uwanja wa Ndege wa Pangkalan Bun, Indonesia leo. wa watu waliokuwa kwenye ndege ya AirAsia ukielea katika Bahari ya Java.… Ndugu na jamaa wa watu waliokuwa kwenye Ndege ya AirAsia wakiwa na simanzi baada ya kupata taarifa za kupatikana kwa miili baharini. Ndugu na jamaa wa watu waliokuwa kwenye Ndege ya AirAsia wakiwa na simanzi baada ya kupata taarifa za kupatikana kwa miili baharini. JITIHADA za kuopoa miili kutoka katika Ndege ya AirAsia QZ8501 iliyoanguka baharini Jumapili iliyopita ikiwa na watu 162 zimeendelea kukwamishwa na hali mbaya ya hewa. Ndege hiyo ilianguka katika Bahari ya Java nchini Indonesia na hali ya dhoruba katika eneo la uokoaji imezidi kukwamisha zoezi hilo. Mamlaka nchini Indonesia yamethibisha kuwa mabaki yaliyoonekana majini eneo la Borneo ni ya ndege iliyopotea ya AirAsia. Rais wa Indonesia, Joko Widodo, ameahidi kuendelea kufanya uchunguzi

bofya hapa ujionee muujiza... KAKAKUONA AONEKANA KIGAMBONI DAR NA KUTABIRI MAKUBWA KWA TANZANIA

Image
Mtoto akiangalia bila woga Kakakuona aliyepatikana nyuma ya nyumba ya Tatu Katala, Mtaa mpya wa Chaboko, Kigamboni Dar es Salaam jana. Mnyama huyo ambaye kuonekana kwake ni nadra inadaiwa ana uwezo wa kutabiri matukio mbalimbali yanayoweza kutokea siku za usoni. Kwa mujibu wa mtoa maelezo ya utabiri huo, Nadhiru Ali alisema siku zijazo nchi itakumbwa na vurugu lakini siyo vita, baada ya mnyama huyo kugusa sarafu, unga na kunywa maji. (PICHA NA KHAMISI MUSSA)  wananchi wakiangalia Kakakuona baada ya kuchukuliwa kwa gari Mpigapicha wa gazeti la Jambo Leo, Khamis Mussa akimshika Kakakuona ili apate neema na baraka  Kakakuona MNYAMA Kakakuona ameonekana Kigamboni, Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine ametabiri mwakani kutokea vurugu lakini si vita. Utabiri huo umekuja siku moja baada ya Mtoto wa aliyekuwa Mtabiri Mashuri Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein(marehemu), Alhaji Maalim Hassan Hussein naye kutabiri kutokea vurugu mwa

PICHA:MAHABUSU AFARIKI AKIJARIBU KUTOROKA KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU

Image
Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba kuna mahabusu alikuwa akijaribu kutoroka kutoka katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu lakini mbinu yake hiyo haikuzaa matunda na hatimaye kuweza kudhibitiwa kwa kupigwa risasi na vyombo vya usalama na kufia hapo hapo. Hizi ni picha zilizochukuliwa kutoka eneo la tukio. 

ESCROW: Kufukuzwa kwa Prof. Tibaijuka, Maovu Mengi Yaanza Kuumbulika…

Image
WIKI moja Kupita Baada ya aliyekuwa Waziri wa Kazi,Nyumba na Mandeleo na Makazi Profesa Anna Tibaijuka kufukuzwa kazi kwenye nafasi hiyo,sasa Mengine mapya yaanza kufichuka kuhusu kufukuzwa kazi kwake,paparazi huru umeelezwa. Taarifa Zinasema Prof Tibaijuka alifukuzwa kazi kutokana na ukosefu wa Maadili kama ambavyo Rais Jakaya Kikwete alivyodai, Rais Kikwete alitangaza kumfukuza kazi Mbunge huyo wa Muleba Kusini (CCM)katika Mkutano wake wa Wazee wanaokaa mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika Mwanzoni mwa wiki liyomalizika jana Jijini Dar Es Salaam,ambapo Rais Kikwete alisema Waziri huyo alipokea zaidi ya Bilioni 1.6 kutoka kwa Mbia wa Kampuni ya IPTL,Bwana James Rugimalira ambapo ni Kinyume na Maadili ya utumishi wa Umma. Licha ya Profesa Tibaijuka kujinadi katika Mkutano wake na Wandishi wa Habari aliouhitisha Alhamisi ya Wiki iliypita na Kujinadi kwamba hawezi kujiuzulu kwenye Nafasi ya Uwaziri kwa Madai hakuhusika kwenye wizi wa zaidi ya Bilioni 306 kwenye Akaunti y

Precision Air Watangaza Nafasi za Kazi Kwa Watu Kumi..Changamkia Deal Haraka

Image
JOB VACANCY Precision Air Services Plc is a quick growing private Tanzanian airline which operates in Partnership with Kenya Airways, with its strategies to expand wings beyond East Africa and Africa. In order to keep our services at a higher level and meet our customers’ maximum satisfaction We wish to invite applications from correctly qualified candidates to fill in this challenging position. POSITION: RESERVATION AND TICKETING SALES AGENT (10 POSTS) REPORTS TO: INDOOR SALES SUPERVISOR DUTY STATION: DAR ES SALAAM – 9 POSTS: ARUSHA – 1 POST ROLE PURPOSE To provide well-organized and effective customer focused Passenger Ticket Sales & Reservation KEY ACCOUNTABILITIES / RESPONSIBILITIES • Make ticket reservations, confirmations, reconfirmations and seat selection for clients on PW flights in compliance with the carrier policies, procedures and customer expectations. • To give fare quotes to all PW clients including group quotations and bookings. • To ensure daily sa

Picha: Gari Lateketea Kwa Moto Maeneo ya Makumbusho Jiji Dar!

Image
Gari dogo aina ya Toyota Mark ii lenye namba za usajili T 601 AHG, likiteketea kwa moto eneo la Makumbusho Usalama kama lilivyonaswa na kamera ya Sufianimafoto jana jioni. Chanzo cha ajali hiyo hakikuweza kufahamika mapema.  Gari hilo likiendelea kuteketea kw moto. Kama kawaida ya wabongo wasiokuwa wanahabari rasmi wakinasa matukio ili kusambaza katika mitandao. Foleni ya magari katika eneo hilo kila dereva akijaribu kushangaa huku moto ukizidi kuliteketeza gari dogo aina ya Toyota Mark ii lenye namba za usajili T 601 AHG eneo la Makumbusho  Raia wakishuhudia tukio hilo wakati gari dogo aina ya Toyota Mark ii lenye namba za usajili T 601 AHG, likiteketea kwa moto. Picha kwa hisani ya Sufiani Mafoto.

KALI YA MWAKA....MTOTO WA MIEZI 3 ABAINIKA KUWA MWATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA HUKO DAR

Image
Mtoto mwenye umri wa miezi mitatu mkazi wa Buza,Dar es salaam amebainika kuwa mwathirika wa dawa za kulevya. Damu na mkojo vya mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa vilichukuliwa na kupimwa katika Maabara ya hospitali ya Mwananyamala na baada ya saa mbili majibu yalitoka yakionyesha kuwa alikua na chembechembe za dawaza kulevya aina ya Heroine. Taarifa za kitabibu ziaonyesha Heroini katika mwili wa binadamu  huweza kuonekana katika mkojo ndani ya siku mbili hadi nne endapo dawa hizo zilitumika na muhusika kwa kati ya saa mbili hadi tano. Mtaalamu wa tibawa hospitali hiyo Elifasi Mritu anasema ‘Ni kweli ukitumia dawa hizo wakati wa kunyoshesha ama ukiwa na mimba mtoto naye huathirika’. Mama wa mtoto huyo Zena au maarufu kama Zerish alisema alipata ujauzito wakati akitumia dawa hizo za kulevya hadi sasa na anapovuta ama kujichoma mtoto wake pia hupata ‘stimu’kwa sababu hupata dawa hizo kupitia maziwa anayonyonya na hivyo wote wawili kulala fofofo sehem

MAMA MJAMZITO ASHIKWA NA UCHUNGU KWENYE TRENI, POLISI WALAZIMIKA KUMZALISHA

Image
Katika siku ya christmas watoto wengi walizaliwa katika siku hiyo, lakini mtoto huyu alizaliwa mazingira ambayo wengi walionekana kushangazwa.  Maafisa wawili wa Polisi Daniel Caban  na Darrell James  walipewa taarifa ya kutakiwa kutoa msaada wa dharura katika treni ya abiria Philadelphia, walipofika waligundua kwamba dharura yenyewe ni mwanamke ambaye alikuwa katika hali ya kukariba kujifungua, muda haukuruhusu kumkimbiza Hospitali. Walimsaidia mwanamke huyo kujifungua salama mtoto wa kiume na baadaye wakapelekwa Hospitali ya Hahnemann University wote wakiwa na hali nzuri. Afisa mmoja amesema alikuwa ameshafungua zawadi zake zote kwa ajili ya siku hiyo na hakujua kama kuna zawadi nyingine ambayo ilikuwa inamsubiria aifungue. Tukio kama hili liliwahi kutokea mwaka jana baada ya mwanamke mmoja kujifungua mtoto wa kike akiwa kwenye treni ya abiria London lakini yeye alipata bahati ya kusaidiwa na mkunga ambaye alikuwa ndani ya treni hiyo pia.

LORI LA MAFUTA LAPATA AJALI MBAYA TANGA

Image
Lori la mafuta likiteketea kwa moto mara baada ya kugonga ngUzo ya umeme huko Handeni mkoani Tanga leo. Wananchi wakishuhudia moto mkubwa uliozuka katika ajali hiyo.PICHA NA GPL

MAMA AMUUA MWANAYE WA KUMZAA ILI AENDE MBINGUNI linsey

Image
Mwanamke mmoja nchini Marekani ameamua kumuua mwanaye wa kiume wa miaka 10 akiamini ataenda mbinguni na kukwepa matatizo ya dunia. Mwanamke huyo mkazi wa mji wa Kansas Lindsey Blansett mwenye miaka 33 alifunguliwa mashtaka ya mauaji baada ya kutenda kosa hilo kwa mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Caleb wakati wakiwa nyumbani na dada yake. Lindsey Blansett na mwanaye Caleb enzi za uhai wake Polisi walisema mama huyo alimkata mtoto wake kwa kutumia kisu bila kujali maumivu aliyoyapata na baada ya kutenda kosa hilo aliwapigia polisi simu ili waweze kumshtaki. Alisema alikua tayari kutumikia adhabu yoyote ile ilimradi ametimiza lengo lake la kumuua mwanaye na kuamini ataenda Mbinguni na kukwepa matatizo ya kidunia ambayo angekutana nayo siku za baadaye.

AUAWA KWA KUCHOMWA KISU NA HAWARA YAKE MDOGO HUKO MOROGORO

Image
Mkazi wa Wilaya ya Kilombero,Morogoro Amon Nyenja amefariki dunia baada ya kuchomwa na kisu na anayedhaniwa kuwa ni hawara wa mke wake mdogo. Ofisa Mtendaji wa kata ya Mang’ula Shabaan Lichaula  na Mkuu wa kituo cha Polisi Nkilijia Lazaro walisema Polisi inamshikilia mwanamke huyo ambaye ni mke wa marehemu wakati wakimsaka mtuhumiwa. Lichaula alidai marehemu katika kumtafuta mkewe alimkuta amesimama mahali na mwanaume huyo na baadaye mwanamke huyo alikimbia na kutokomea na marehemu kuamua kumvaa mgoni wake lakini alizidiwa baada ya mtu huyo kumchoma kisu cha ubavuni hadi utumbo kutoka nje. Alisema baada ya marehemu kuchomwa kisu alipiga kelele za kuomba msaada na wasamaria wema walijitokeza na kumwahisha hospitali na alifariki dunia baada ya kufanyiwa huduma ya kwanza wakati akihamishiwa katika hospitali Mtakatifu Fransis,Ifakara kwa matibabu zaidi.

UMEISIKIA HII YA WALE WATUHUMIWA WALIOMUUA DKT SENGONDO MVUNGI?

Image
Washtakiwa 11 wa kesi ya mauaji ya kukusudia ya aliyekua mjumbe wa tume ya mabadiliko  ya Katiba,Dk Sengondo Mvungi jana waligoma kwa muda kuondoka kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakishinikizwa kuelezwa lilipo jalada la kesi yao na hatua ilipofia. Hilo lilitokea jana saa nne asubuhi ,muda mfupi  baada ya wakili wa serikali,Peter Njikekumweleza Hakimu Hellen Liwa kuwa kesi hiyo ilifika mbele yake kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake bado haujakamilika na kuomba ipangwe tarehe nyingine. Mshtakiwa Masunga Makenza alidai hafahamu sheria ,kesi hiyo ni ya muda mrefu na akahoji jalada likienda kwa DPP linatakiwa kukaa kwa muda gani. Makenza alidai kuwa kesi hiyo ni ya kubambikiwa na kwamba ingekuwa halisi,upande wa mashtaka ungekuwa umekwishakamilisha upelelezi na kwamba wapotayari kushtakiwa ila kama upande wa mashtaka umeshindwa kukamilisha upelelezi mahakama iwaachie huru na ikikamilisha iwakamate tena.

MVUA ILIYONYESHA JANA JIJINI DAR YASABABISHA VIFO

Image
Mvua iliyonyesha jijini Dar es salam imeleta balaa baada ya kuua watu wawili katika maeneo tofauti ya jiji hilo likiwemo tukio la mtoto wa miaka minne kufa baada ya kuzidiwa na maji yaliyoingia ndani ya nyumba wakati akiwa amelala. Kwa mujibu wa Taarifa ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar Camilius Wambura alisema matukio hayo yalitokea jana mchana kwenye maeneo mawili tofauti. Tukio la kwanza lilitokea eneo la Tandale ambapo mtoto Nasma Ramadhani akiwa amelala ndani ya nyumba yao maji ya mvua yaliingia ndanina kumzidia nguvu hadi kufariki na mwingine bibi kizee kufariki eneo la Mwananyamala aliyeangukiwa kichwani na ukuta wa nyumba yake na kumsababishia mauti. Wambura alisema madhara mengine ni maji kujaa kwenye ameneo mbalimbali ikiwemo Mikocheni zilizopo ofisi za Tanesco,Kinondoni jirani na TMJ hivyo kuleta usumbufu wa Magari na watukuvuka eneo hilo.

AIBU KUBWA.....MAMA MZAZI APEWA MIMBA NA MTOTO WAKE WA KUMZAA MARA MBILI MFULULIZO momaaaaa

Image
Duniani kuna vituko,hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya mama mmoja kubeba mimba ya mtoto wake mara mbili mfululizo. Tukio hilo lilitokea nchini Zimbabwe baada ya mama mmoja ajulikanaye kwa jina la Ethel Vhangare kuwa katika mahusiano na mtoto wake Simon Matsavara wakati mume wake akiwa anaugua ugonjwa wa kupooza. Kwa mara ya kwanza Simon alimpa ujauzito mama yake lakini baadaye mimba ilitoka wakati ikiwa na miezi mitano siku chache kabla ya kifo cha mumewe Agripah Matsava na kutangaza kwa majirani zake kuwa mimba hiyo ni ya mtoto wake Simon. Baada ya majirani kupata taarifa hiyo waliamua kumshtaki mama huyo na mwanaye kwa wazee wa mila ambapo walipewa adhabu ya kulipa mifugo mingi kama faini.. Licha ya kifo cha mume wake wawili hao waliendelea na mahusiano yao kama kawaida na ndipo alipopata mimba nyingine ambapo waumini wenzake walishtukia baada ya kushindwa kuhudhuria kanisani na kuamua kwenda kumtembelea na ndipo walipogundua ni mjamzito tena n

Maandalizi ya kujifungua salama kwa mama Mjamzito…

Image
Shirika la Afya Ulimwenguni linasema; kila siku karibia wanawake 800 hufa kwa matatizo ya mimba na uzazi yanayoweza kuzuilika. Asilimia 99 ya vifo vya kina mama wajawazito hutokea kwenye nchi zinazoendelea. Nusu ya vifo hivi hutokea nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, ikiwemo na Tanzania. Hatari ya vifo vya kina mama wajawazito ni kubwa zaidi kwa mabinti walio na umri chini ya miaka 15 na matatizo wakati wa ujauzito na kujifungua ndio chanzo kikubwa cha vifo hivyo. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni, mwaka 2013 wanawake 289,000 walikufa kwa matatizo ya mimba na uzazi. Uwiano wa vifo vya kinamama wajawazito katika nchi zinazoendelea kwa mwaka 2013 ni vifo 230 kwa kila vizazi hai 100,000 wakati ni vifo 16 tu kwa kila vizazi hai 100,000 kwa nchi zilizoendelea. Kadiri mwanamke anavyofahamu mambo mengi zaidi kuhusu mimba yake ndivyo alivyo na nafasi nzuri ya kufanikiwa kujifungua kwa usalama. Kwa kujitunza kabla na wakati wa kujifungua na kufikiria ki