Diamond Hana Uwezo wa Kumpa Mwanamke Ujauzito


BAADA ya kudaiwa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa alichoropoa mimba zake mbili, mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’ ameibuka na kujibu mapigo kwamba mwanamuziki huyo hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba.

Akizungumza na GlobalTV Online  hivi karibuni, Diamond alifunguka: “Nilimpa (Penny) mimba ya kwanza, sikuamini ikabidi twende naye hospitalini tukapime, akaambiwa anayo…nikafurahi nikampiga na ndinga (gari) mpya siku hiyohiyo, nikamwambia mama tulia unizalie mwanangu.

“Sikukaa sana akaniletea maneno…oooh mara hivi mara vile…eti imetoka. Nikasema poa, labda haikuwa riziki. Nikampa ya pili, nayo pia akatoa. Nikasema bora niachane naye na huo ndiyo ukawa mwisho wa mimi na Penny.”

Baada ya habari hiyo kusambaa Penny alijibu mapigo na kudai kwamba ni kweli staa huyo alikuwa akimridhisha kimapenzi lakini hakuwa na uwezo wa kumpachika mimba kama alivyodai.“Diamond ni mwanaume kama wanaume wengine lakini hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba, muulizeni vizuri tatizo ni nini,” alisema Penny.

Alipofikishiwa taarifa hizo, Diamond hakutaka kufunguka kwa madai kwamba kuna vitu huwa hataki kuvisema kwa kuwa ni mtoto wa kiume na huwa anahifadhi siri nyingi za wanawake.

Kwa mujibu wa Penny ni kwamba alikuwa akimridhisha vizuri kimapenzi hivyo hana tatizo la nguvu za kiume isipokuwa hawezi kumpa mwanamke kibendi.

Akizungumzia tatizo la Diamond (kama maelezo ya Penny ni kweli), mtaalam wa masula ya tiba ya uzazi  alisema kuwa mwanaume anaweza kumridhisha vizuri mwanamke wanapokuwa kitandani isipokuwa akashindwa kumpa ujauzito.

“Tatizo la kutopata ujauzito, maana yake mume na mke walio katika uhusiano wa kutafuta mtoto ndani ya mwaka mmoja, lakini wameshindwa.
 
“Inaweza ikawa zaidi ya mwaka mmoja lakini wastani wa kiwango cha chini ni mwaka mmoja.
 
“Ni tatizo kubwa katika jamii kwani kila mmoja anataka afikie malengo ya kuwa na familia kama anavyotaka Diamond.
 
“Mwanamke na mwanaume wote wanahusika katika tatizo hili japo mara nyingi huonekana ni la mwanamke."

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini