BAD NEWS: AJALI Yasababisha Mshindi wa Miss Universe Tanzania 2014 Kutoenda Mashindano ya Dunia!

Kamati ya Miss Universe Tanzania
imemteua mshindi wa pili wa Miss
Universe 2014, Nale Boniface kwenda
kuiwakilisha nchi katika mashindano ya
kimataifa ya Miss Universe
yatakayofanyika mwanzoni mwa mwezi
wa kwanza 2015 Miami, Marekani.
Taarifa rasmi inasema hatua hii
imechukuliwa baada ya mshindi husika
Miss Universe Tanzania 2014 Carolyne
Bernard kupata ajali na kuvunjika kidole
chake cha mguu.
Ripoti ya daktari imeonesha kuwa
kupona kwake kutachukua mwezi
mmoja wakati mrembo anatakiwa awe
mashindanoni baada ya siku kumi
kuanzia sasa na isitoshe awapo
mashindanoni mrembo atapaswa kuvaa
viatu virefu (High heels) wakati wote
ambapo haishauriwi kiafya kutokana na
tatizo lake.
Kutokana na hali hii, Nale Boniface
ambaye alishika nafasi ya pili na
kuiwakilisha Tanzania katika
mashindano ya Miss Earth ndiye
atakayekwenda kuiwakilisha nchi badala
yake kama mkataba unavyoainisha na
hivyo atakuwa Miss Universe Tanzania
2014.
Kamati inasikitishwa na kuumia kwa
Carolyne na inaahidi kuendelea kuwa
nae bega kwa bega katika matibabu yake
kwani bado yupo chini ya mkataba wa
Miss Universe Tanzania kwa mwaka
mzima.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania
mwaka huu yalifanyika tarehe 31 mwezi
wa kumi.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini