DUNIA HAINA HURUMA: AKIMBIWA NA MUME KWA KUZAA MTOTO MLEMAVU!

DUNIA HAINA HURUMA! Mwanamama
mmoja aliyejitambulisha kwa jina la
Sarah Lyimo, mkazi wa Buza Mwang’ati
jijini Dar es Salaam amejikuta kwenye
wakati mgumu baada ya mumewe
aitwaye Mohammedi kumkimbia baada
ya kile alichodai kuwa na mtoto mwenye
ulemavu.
Akizungumza na mwandishi wetu wiki
iliyopita kuelezea mkasa mzima wa
kutelekezwa  kwake, Sarah alidai aliishi
na mwanaume huyo ambaye ni dereva
wa bodaboda kwa miaka minne na
kufanikiwa kuzaa naye watoto wawili
hapa Dar.
Akifafanua zaidi Sarah alisema:
“Mwanzoni tulipendana sana na mume
wangu. Mtoto huyu nilipomzaa alikuwa
hana tatizo lolote, alianza kukumbwa na
matatizo kwa kuumwaumwa akiwa na
miezi sita ndipo akaanza kubadilika na
kupatwa na ulemavu wa miguu na
mikono.
“Eti ndugu wa mume wanasema kwa
kuwa tumempa jina la marehemu babu
yake bila ridhaa ya bibi yake ambaye
yupo hai ndiyo maana mtoto amelemaa,
wakaniambia inabidi twende kaburini
tukamuombe radhi (babu yake) ndipo
mtoto atapona. Mimi sina imani hizo.
“Balaa lilizidi siku hadi siku kwa baba
yake kutomjali mtoto huyo kwa matunzo
yoyote na kunikashifu akidai eti mtoto
wake hawezi kuwa kilema, hata hivyo
tulikuwa tukiishi kwa tabu nikapata
mimba na mwanzoni mwa mwaka jana
nikaenda kujifungulia kijijini kwetu
Moshi, niliporudi nikakuta anaishi na
mwanamke mwingine, ndipo aliponiacha
na sasa nimebaki nahangaika, pa kuishi
sina naishi na wanangu kwa marafiki,
amenitelekeza.”
Alisema kutokana na ugumu wa maisha
alionao anadhani bora arudi kwao
Moshi, kuliko kuendelea kuteseka
kwenye jiji asilolifahamu vizuri.
na mume wake, Mohammedi.
“Nawaomba Watanzania wanichangie
fedha ya nauli ya kurudi kwetu pia
waniwezeshe mtaji ili nikaanzishe mradi
wa kujikimu kimaisha na wanangu,”
alisema Sarah.Wakati Uwazi linakwenda
mitamboni, Sarah alisema mtoto huyo
amefariki dunia Ijumaa iliyopita.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini