Anna Tibaijuka: A Disgrace to Academia (Fedheha kwa Wanazuoni)

Anna Tibaijuka alikuwa profesa UDSM kabla ya kujiunga na uanaharakati (BAWATA), UN na baadaye siasa. Kwa vile bado anatumia cheo cha uprofesa, ni matarajio ya kila mtu kuwa ataishi na kutenda kulingana na matakwa na maadili ya uprofesa. Lakini majukumu ya profesa ni yapi?

 Katika taasisi za elimu ya juu, maprofesa hufundisha ktk ngazi zote; hubuni mitaala; hufanya na kusimamia tafiti mbalimbali na kutoa machapisho; hutayarisha bajeti nk. Maprofesa huongozwa na kanuni hii ya msingi: uaminifu, uadilifu na huduma kwa binadamu (service to mankind). 

Ni jambo ambalo halifikiriki kusikia kwa mfano profesa hakutoa utahini wa haki (fair evaluation) au ameiba kazi za wengine (plagiarism) kwa kichocheo (motive) chochote. Duniani kote, profesa ni mtu wa hadhi na heshima (noble standing). Kwa vile Anna Tibaijuka ameshindwa kuishi kwa kuzingatia hii misingi akiwa katika siasa, kwa kuendeleza ubinafsi na ufisadi yafuatayo yanapaswa kufanyika mara moja:

 1. Baraza la UDSM limvue uprofesa
 2. UDASA wamkane (disown)


Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini