UGONJWA WA MALARIA KWA MJAMZITO

Malaria ni maambukizi ya seli nyekundu
za damu inayosababishwa na vimelea
vinavyoitwa kitaalamu, Plasmodiumu.
Plasmodiumu hawa husambazwa na
mbu aina ya Anofelesi. Mbu hutoa
parasiti za malaria na kukomaa katika
seli nyekundu za damu na mamilioni ya
parasiti hukusanyika katika plasenta ya
mjamzito. Malaria ni hatari zaidi kwa
wajawazito kuliko watu ambao hawana
mimba.
Dalili za malaria
Mama mjamzito anakuwa na dalili kama
wagonjwa wengine ambao siyo
wajawazito ambapo atajisikia baridi na
kutetemeka, maumivu ya kichwa, mwili
kuwa na joto kali, kutokwa na jasho joto
lishukapo, kuhara au kutapika au kuwa
na maumivu ya misuli au viungo.
Vipimo vya malaria
Malaria huweza kugundulika kwa
kutumia vipimo vya haraka au darubini.
Matibabu kwa mjamzito
Ni muhimu kwa wajawazito kuepukana
na malaria au kutibiwa haraka wakiwa
wagonjwa. Dawa za kutibu malaria
zinaweza kuwa na madhara lakini ni
afadhali kuliko kupatwa na malaria.
Ikiwa mama ana dalili za malaria,
anapaswa kutibiwa mara moja kwa
kumuona daktari.
Wiki 12 za awali za ujauzito mama akiwa
na malaria atatibiwa kwa Kwinini na
Clindamycin au Kwinini pekee iwapo
Clindamycin haipatikani. Dawa hizi
zikishindwa kutibu Artesunate hutumika
katika matibabu kwa muda wa siku saba.
Lakini dawa mseto jamii ya Artemisin
zinaweza kutumika kutibu malaria
ambayo siyo kali.
Mjamzito aliye na malaria anaweza
kupata madhara kwa kuharibika mimba,
kuzaa njiti, kuzaa mtoto aliyekufa au
kufa yeye mwenyewe.
KINGA: Mjamzito afanye kila awezalo
kuepuka kuumwa na mbu kwa kutumia
chandarua, kupuliza dawa na
kuangamiza mazalia ya mbu au kuchoma
dawa ya kuua mbu.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini