AFYA YAKO! TAMBUA VIMBE MBALIMBALI KWA MWANAMKE NA JINSI YA KUZIONDOA PASIPO UPASUAJI-2

Wiki iliyopita tuliziangalia aina za vimbe
mbalimbali katika mwili wa mwanamke
na tukaziweka wazi ili kila mtu aweze
kuzijua na kuzielewa. Lakini changamoto
ni moja nayo ni kwamba mtu hawezi
kujua kama ana vimbe au laa hadi aweze
kufanya vipimo, lakini kuna baadhi ya
dalili ambazo zinaweza kukujulisha au
kukushitua kwamba wewe una dalili
moja au mbili za vimbe.
DALILI ZA VIMBE KATIKA MWILI WA
MWANAMKE
Kuna dalili tofautitofauti katika mwili wa
mwanamke zinazoashiria kuwa
mwanamke huyu ana vimbe, na dalili
hizo ni kama;
Ovarian Cysts, tutaanza na dalili
zinazoweza kukuonyesha kuwa wewe
una ovarian cysts yaani uvimbe
unaotokea juu ya kifuko cha mayai ya
uzazi, inaweza ikawa ni upande mmoja
au pande zote mbili, na dalili hizo ni
kama;
Maumivu ya kichomi au kama kichomi
chini ya kitovu na maumivu haya huwa
hayawi kwa marefu hapana yanakuwa
sehemu moja tu na yanakuwa kama
kichomi. Na maumivu haya yanaweza
kuwa ya upande mmoja au pande zote
mbili na mara nyingi hutokea pale mtu
anapokuwa akicheka au kuinama au
akiwa unakimbia au ameinua kitu kizito,
hiyo inakuonyesha kuwa wewe una
ovarian cysts.
Dalili nyingine ni kuvurugika kwa hedhi,
ukishaona unaandamwa na matatizo ya
hedhi na vichomi sehemu za chini ya
kitovu basi ujue unaandamwa na ovarian
cysts au vimbe katika kifuko cha mayai.
Napoongelea kuvurugika kwa hedhi basi
nina maana kuwa unapata hedhi mara
kwa mara, au hedhi kidogo sana au
hedhi nyingi sana na maumivu ya
kichomi basi inakuwa ni ovarian cysts.
Kutokwa na uchafu sehemu za siri, pia
mwanamke anayetokwa na uchafu
sehemu za siri na uchafu huo ukawa
hauna harufu na wala hauna miwasho ya
aina yoyote ile basi anakuwa
anaandamwa na ovarian cysts.
Fibroids au Mayoma, na hizi ni vimbe
zinazotokea katika mji wa mimba na hizi
ndizo vimbe zinazowasumbua watu
wengi sana  katika jamii yetu ya sasa, na
dalili zake ni kama;
Hapa mwanamke hupatwa na maumivu
chini ya kitovu lakini ni katikati siyo
upande wa kulia wala upande wa
kushoto na mara nyingi maumivu haya
huambatana na maumivu ya kiuno,
maumivu ya mgongo na maumivu hayo
huenda hadi sehemu za mapaja na
kushuka hadi miguuni na maumivu haya
huwa makali sana hasa wakati wa hedhi.
Sasa ukiona unaandamwa na dalili hizi
basi ujue kuna uwezekano ukawa na
Fibroids au Mayoma.
Kuongezeka kwa ukubwa wa tumbo,
mwanamke ukiona tumbo linaongezeka
ukubwa na unasikia kama kuna kitu
kinatembea ndani ya tumbo, wakati
huohuo unaandamwa na maumivu
makali chini ya kitovu kwa katikati na
maumivu makali sana wakati wa hedhi
basi ni dalili kubwa sana nawe ukawa na
Fibroids au Mayoma.Kwa maana hiyo
basi sote tutakuwa tumetambua dalili
mbalimbali za vimbe katika mwili wa
mwanamke kwenye upande wa ovarian
cysts na mayoma.
Itaendelea wiki ijayo.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini