DIAMOND AMSIFU DAVIDO...KRISMASI NAYE YUPO DAR LIVE!

WIKI iliyopita tuliishia pale ambapo staa
wa Bongo Fleva, Diamond aliachia video
yake ya Number One katika uzinduzi
usiyo na kiingilio alioufanya ndani ya
Hoteli ya Serena jijini Dar ambapo pia
alimzawadia gari, aliyekuwa
mwanamuziki nguli nchini, marehemu
Muhidin Maalim Gurumo.
Wiki hii tunaendelea ambapo katika
kuanika maisha yake,
ASIFU KAMPANI YA DAVIDO
“Mwezi wa 10, 2013 nilifanya kolabo na
Davido (David Adedeji Adeleke) kutoka
nchini Nigeria katika video ya Number
One remix halafu nilifunga safari hadi
Nigeria lengo likiwa ni kuangalia masoko
ya muziki katika nchi za wenzetu.
“Naweza kusema wimbo wa Number
One ndiyo uliweza kunitambulisha
kimataifa, nilipata mashabiki kibao na
kushiriki kwenye tuzo za kimataifa
ikiwemo MTV Mama nchini Afrika Kusini
ambapo nilipanda jukwaani na Davido.
Kuna tuzo nyingine kama BET,
Afrimama, MTV Europe Channel O,”
alisema Diamond.
Julai 7, mwaka huu, Diamonnd
alimzawadia gari mama yake aina ya
Toyota Lexus pia aliachia video mbili za
Mdogomdogo iliyofanyika nchini
Uingereza na Bumbum aliyomshirikisha
Iyanya kutoka Nigeria aliyoifanyia Afrika
Kusini. Video hizi anasema zilimgharimu
dola 78,000 za Marekani.
KUTUA DAR LIVE KRISMASI
Hivi karibuni, Diamond alikuwa nchini
Uganda kwenye shoo ya nguvu ya
mwanamuziki wa nchi hiyo, Zarina
Hassan ‘Zari’ lakini amerudi Bongo
haraka sana kwa sababu keshokutwa
(Alhamisi) anapanda kwenye jukwaa la
Ukumbi wa Kimataifa wa Burudani wa
Dar Live, Mbagala-Zakhem kwa ajili ya
kutoa raha ya Sikukuu ya Krismasi.
Diamond atapanda na Mzee Yusuf wa
Kundi la Jahazi Modern Taarab.
Anaitwa Diamond Platnumz, mzaliwa wa
Kitongoji cha Tandale kwenye Jiji la Dar
es Salaam, ameweza kukitumia kipaji
chake vizuri na kupata mafanikio
makubwa sana. Hongera sana Diamond.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini