BIBI KIZEE ADONDOKA NA UNGO AKITOKA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA KRISMAS HUKO KAHAMA

Wakazi wa Bukondamoyo katika Halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga wameingiwa na hofu baada ya bibi kizee mmoja kudaiwa kudondoka kwenye ungo akidaiwa kutoka mkoani Tabora kusherekea sikukuu ya Chrismas.

 Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo lililokusanya umati mkubwa wa watu wamedai bibi kizee huyo alidondoka alfajiri huku akidai alikuwa na wenzie watano ambao walifanikiwa kutoroka kuelekea kijiji cha Ndugu kata ya Kinaga wilayani Kahama.

 Aidha bibi kizee huyo baada ya kuhojiwa na mwandishi wa habari hizi alisema anaitwa Chausiku huku akidai alikuwa akielekea katika kijiji hicho cha Ndugu.

 Hata hivyo jeshi la polisi wilayani Kahama liliwahi kufika kwenye tukio na kumuokoa bibi kizee huyo ambaye alionekana kuvaa nguo zilizochakaa na makovu katika mkono wake wa kushoto ambapo imedaiwa alichubuka wakati akidondoka.

 Tukio hilo limehusishwa na imani za kishirikina kwa kuwa ungo ni kifaa kinachoaminiwa kutumika kwa nguvu ya giza kupaa angani kama usafiri unaotumiwa na wanga katika shughuli zao za nguvu ya giza ikiwemo uchawi.

Na Shija Felician - Kahama.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini