Posts

Showing posts from 2015

Picha,Shilole kafuta tattoo ya Nuh Mziwanda kwenye kifua na kuweka hichi.

Image
Msanii wa muziki wa bongo fleva Shilole ambaye alikuwa kwenye mahusiano na Nuh Mziwanda amefuta tattoo ya jina la mpenzi wake Nuh Mziwanda iliyokuwa imechorwa kwenye kifua chake. Hii imekuwa ishara kamili kuwa wasanii hawa kwa sasa hawako pamoja kama ilivyokuwa awali .       ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!! LIKE PAGE  YETU KWA  HABARI  ZAIDII

HOW TO WEAR BOLD PRINTS

Image
how they wore the prints kwa runway kama hujui jua leo kuwa a blazer can be belted ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!! LIKE PAGE  YETU KWA  HABARI  ZAIDII

mishono mipya 2016

Image
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!! LIKE PAGE  YETU KWA  HABARI  ZAIDII

Mtukaneni tu Tiffah Lakini Siku Moja Atakuja Kuwa Rais Wenu – Zari

Image
Watu hawana haya – Kwa mujibu wa Zari the Bosslady, baadhi yao wamekuwa wakimporomoshea matusi mtoto wake aliyezaa na Diamond, Tiffah tangu alipozaliwa. Lakini Zari ana habari kwa haters! Mrembo huyo wa Uganda anaamini kuwa siku moja watamheshimu mtoto wake sababu anamlea aje kuwa rais kama Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia! “Matusi from day one even before she was born,” ameandika Zari kwenye Instagram. “But she is here and strong enough to handle. Boss ladies use bricks thrown at them to build empires. And this right here is my future president in the making #IronLady #EllenJohnsonSirleaf #Kichuna @princess_tiffah.” ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!! LIKE PAGE  YETU KWA  HABARI  ZAIDII

Shilole Aporomosha Matusi Hewani Akihojiwa Redioni Baada ya Kuulizwa Kuhusu Kuachana na Nuhu Mziwanda..Mashabiki Wadai Amefanyiwa Interview Akiwa Mlevi

Image
MWIGIZAJI na mwanamuziki wa kizazi kipya Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amemzingua Dj Tass mtangazaji wa kipindi cha Kwetu Fleva baada ya kushusha matusi hewani akihojiwa na mtangazaji huyo na kumfanya aombe msamaha kwa wasikilizaji kwa kutamka Sorry for That mara mia. Tass alikatiza matangazo baada ya Shilole kuulizwa swali kuhusu mpenzi wake Shilole ambaye ametangaza kutengena naye hivi karibuni Mziwanda ambaye alitamba naye kwa muda mrefu na hata msanii huyu wa kiume kujichora picha ya Shilole mwilini mwake. “Wapenzi wa kipindi cha Kwetu Fleva nawaomba radhi kwa kilichotokea Shilole waombe msamaha, na nimekukanya mara ngapi? Nitakuzingua upo hewani unatukana una maananisha nini? Sorry for that, sorry for that,”anasema Dj Tass. Baada ya kuagana na Shilole wapenzi wa kipindi hicho wamelaumu Dj Tass kwa kumleta Shilole akiwa kalewa studio na kuharibu interview , msanii huyu alikuwa akimponda sana Nuhu Mziwanda akimtangaza msanii kutoka Uganda E Kenzo kama mchumba wake mpya ...

AY: Wazungu wamenitibulia sapraizi

Image
Ambwene Yesaya ‘AY ‘. Gabriel ng’osha Hii nayo kali! Unajua AY na ngoma yake iitwayo Zigo, sasa basi jamaa alifanya remix ya wimbo huo akimshirikisha Diamond kisha kutaka kufanya sapraizi kwa Wabongo. Unajua kilichotokea? Unaambiwa Wazungu ambao ndiyo waliotengeneza kichupa cha wimbo huo wakawapiga picha kisha kuziachia mtandaoni, kitendo kilichotibua kila kitu. “Nilitaka kufanya sapraizi kwa kufanya video ya wimbo huo kwa siri kisha kuja kuiachia kwa kuwashtukiza. Kumbe bwana Wazungu wametupiga picha bila sisi kujua na kuzitupia mitandaoni, yaani wametibua mambo mwanangu,” alisema AY. ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!! LIKE PAGE  YETU KWA  HABARI  ZAIDII

Kidoa amtangazia vita Zari

Image
Video Queen maarufu Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’. Musa mateja Video Queen maarufu Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’ amemtangazia vita mpenzi wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ akidai atafanya kila njia amnase msanii huyo. Rafiki wa karibu wa Kidoa aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini alidai kuwa, Kidoa alikuwa akimpenda sana Diamond hata kabla ya kuwa na Zari ndiyo maana ana ndoto za kuwa naye. Mpenzi wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’. “Kidoa anamzimia sana Diamond, achilia mbali kumpenda kutokana na kazi yake ya muziki lakini pia kimapenzi, maana kuna wakati anakosa raha kabisa anapowaona Zari na Diamond wakiwa kimahaba,” anadai mtoa habari huyo. Katika kujua ukweli wa habari hii, mwandishi wetu alimtafuta Kidoa ambapo bila kuficha alianika hisia zake kwa kusema: “Kiukweli nampenda sana, najua Zari hawezi kujisikia vizuri kusikia maneno haya lakini ndiyo hivyo na niko tayari kwa lolote… “Nilipotangazwa kuwa msanii mwe...

Mke alivyomuua mumewe kikatili na kumfukia!

Image
Mwanamke aliyezungushiwa duara jekundu ndiye anayedaiwa kumuua mumewe na kumfukia. NI simulizi ya kushangaza kufuatia Archard Frederick (41), kudaiwa kupigwa na kitu kizito kichwani hadi kufariki dunia na mkewe, chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi. Tukio hilo lilijiri Desemba 11, mwaka huu Kijiji cha Irogelo, Kitongoji cha Buhesi, Kamachumu, Muleba, Kagera. Akizungumza na gazeti mwenyekiti wa kijiji hicho, Prudence Rutaihwa alisema kabla ya Archard hajafariki dunia aligombana na mkewe. Alisema marehemu alipotea ghafla jioni ya Ijumaa ya Desemba 11, mwaka huu saa 12 jioni. “Jumamosi asubuhi wafanyakazi wenzake wa ujenzi walimpitia kwake ili waende kibaruani wakakuta mlango umefungwa. Walipompigia simu hakupatikana hewani, wakaondoka. Alisema wenzake hao walijua watoto walikwenda machungani na mkewe alikwenda shamba lakini baada kutopatikana hewani, kaka wa marehemu, Projest Fredrick alipewa taarifa na kuanza kuwa na wasiwasi. Kaburi alilozikwa ma...

Matatizo yanayowafanyawaugue mara kwa mara

Image
Watoto wanaopatwa na matatizo ya kuugua mara kwa mara ni wale walio katika umri wa chini ya miaka mitano. Watoto hawa huumwa na wanapogundulika kuwa ni wagonjwa tayari hali inakuwa mbaya. Hii ni kwa kuwa watoto hawa hawana uwezo wa kujieleza mara tu wanapopata dalili za awali za ugonjwa. Pamoja na yote, magonjwa au maradhi ya watoto huanzia mbali sana kama tutakavyokuja kuona. Inawezekana kabisa mtoto asiugue na akaishi vizuri kuanzia anapozaliwa hadi anavuka umri wa miaka mitano. Matatizo mengi ya kiafya kwa watoto hupunguza umri wao wa kuishi au huwadhoofisha kimwili na kiakili na kusababisha wasikue vizuri na hata uwezo wao wa kujifunza mambo mbalimbali ya kimaisha katika familia au darasani hupungua. Kwa mujibu wa takwimu mbalimbali katika jamii nyingi hapa Afrika Mashariki, watoto wapo kwa idadi kubwa kuliko watu wazima na inakadiriwa watoto ni asilimia 50 ya watu wazima lakini watoto 250 kati ya 1000 wanaozaliwa hufariki kabla hawajasheherekea bethidei yao y...

Ndege ya abiria ilivyokatiza safari yake angani kisa Panya..

Image
Matukio yameendelea kuchukua headlines India.. ukiachia lile tukio la joto kali lililofanya watu kushindwa kuvumilia na kukaa ndani ya maji wakihofia maisha yao huku wengine wakipoteza maisha kutokana na joto kali kuna hii nyingine imetokea huko. Ndege ya Air India ambayo ilikua ikitoka Mumbai kuelekea London, Uingereza ililazimika kugeuza safari ikiwa na abiria wake 171 na kurudi ilipotoka baada ya abiria kubaini kuwepo kwa panya ndani ya ndege hiyo. Ingawa juhudi za kumpata panya huyo ziligonga mwamba lakini rubani alilazimika kurudi Mumbai ili kuwatoa wasiwasi abiria zaidi ya 170 waliokuwa wakisafiri kwa kutumia ndege hiyo ya shirika la ndege la India. Baada ya kutua abiria walilazimika kubadilishiwa ndege na kuanza safari upya ya kuelea London. ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!! LIKE PAGE  YETU KWA  HABARI  ZAIDII

Video-Wamekaa wanasubiri mwaka mpya, ghafla moto umezuka hotelini Dubai..

Image
Wakati unahesabu dakika chache kuuvuka mwaka 2015 salama, najua kuna watu wangu wako kwenye nyumba za ibada wanamshukuru MUNGU, wengine wamekusanyika na ndugu jamaa na marafiki kwa utulivu kuenjoy huku wakisubiri na kuzihesabu kwa pamoja zile sekunde za mwisho za mwaka 2015 kwa amani kabisa, inanifikia taarifa kutoka Dubaikwamba jingo moja la Hoteli limewaka moto ghafla !! Moto umeonekana kuwaka kwenye jengo la ghorofa lenye urefu wa mita 300 ambalo liko jirani na jengo refu la Dubai, Burj Khalifa huku watu wengi wakikusanyika kushuhudia tukio hilo. Taarifa za mwanzo zimesema watu 16 ni majeruhi, vikosi vya zimamoto vimefanya kazi yao pia kuudhibiti japo chanzo cha moto hakijafahamika… Stori ninayo kwenye video hapa. ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!! LIKE PAGE  YETU KWA  HABARI  ZAIDII

Hii ndio list ya magoli 10 bora yaliofungwa kwa mwaka 2015, Cheki video hapa …

Image
Mtu wangu wa nguvu hongera na kheri ya mwaka mpya, licha ya kuanza kwa mwaka 2016 ila mwaka 2015 ulikuwa na mambo mengi ya kukumbukwa katika kila kitu. ila mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee TOP 10 ya magoli 10 bora yaliofungwa kwa mwaka 2015. Stori kutoka 101greatgoals.com hii ndio list ya magoli yenye mvuto na ufundi. 1- Alessandro Florenzi wa AS Roma alifunga goli hili katika mechi dhidi yaFC Barcelona. 2- Lionel Messi alifuga goli hili katika mchezo dhidi ya Athletic Bilbao. Hili ni moja kati ya magoli matatu bora ya FIFA kwa mwaka 2015. 3- Carli Lloyd (United States) v Japan 4- Bernard Bulbwa (Nigeria U20) v Senegal 5- Michél Harrer (VfR Neumünster) v Havelse 6- Marcel Ndjeng (SC Paderborn) v Bolton 7- Philippe Mexes (AC Milan) v Inter Milan 8- Japanese high school team 9- Cuco Martina (Southampton) v Arsenal 10- Miguelete Ramírez (Barcelona U15) v La Floresta. Hili limeingia kutokana na umahi...

Hivi ndivyo Chicharito alivyozidi kumtia aibu kocha wa Man United Louis van Gaal …

Image
Mshambuliaji wa kimataifa wa Mexico anayekipiga katika klabu ya Bayer Leverkusen yaUjerumani Javier ‘Chicharito’ Hernandez, December 31 amerudi tena katika headlines za soka, baada ya mafanikio yake kuzidi kuonekana. Chicharito amerudi kwenye headlines baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi. Kufuatia kushinda tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mwezi, hii inatafsirika kama ishara aibu kwa kocha wa Man United Louis van Gaal ambaye alisababisha kuondoka kwa mchezaji huyo, kutokana na kauli yake ya kutompa nafasi ya kucheza na kumwambia kuwa hana nafasi katika kikosi chake. Chicharito aliyeondoka Man United katika dirisha dogo la usajili la mwezi August 2015, ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa wezi mara mbili mfululizo, baada ya mwezi November kufanikiwa kutwaa tuzo hiyo. Kwa sasa Chicharito amecheza jumla ya mechi 14 akiwa na klabu ya Bayer Leverkusen na kufanikiwa kushinda jumla ya goli 11, wakati mshambuliaji tegemeo wa Man UnitedWayne Ro...

Magazeti ya Tanzania January 1, 2016 na stori zake kubwa kurasa za mwanzo na mwisho

Image
Leo January 1, 2016   nimekuwekea tena stori zote kubwa za Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye Udaku, michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea mtu wangu, usiache kukaa karibu yangu kwenye facebook twitter na instagram  winternews1.blogspot  ili niwe nakutumia kila kinachonifikia. . . . . . . . . . . . . . . . . . ® . . . . . . . . . ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!! LIKE PAGE  YETU KWA  HABARI  ZAIDII