Neymar athibitisha Manchester City kutaka kumsajili




Na Rabi Hume, Modewjiblog

Staa wa Brazil na klabu ya Barcelona, Neymar (pichani) amethibitisha kuwa anafahamu kwa Manchester City inahitaji saini yake ili ajiunge na klabu hiyo ya nchini Wingereza.

Neymar ambaye kwa sasa yupo katika harakati za kufanya mazungumzo na klabu yake ya Barcelona kuhusu kuongeza mkataba alisema kuwa Manchester City imekuwa ikionyesha nia ya kutaka kumsajili hasa katika kipindi hiki ambacho haifahamiki kama ataendelea kusalia Barcelona au atageuza upepo na kuelekea klabu nyingine.

Akiwasili katika uwanja wa ndege wa El Prat uliopo jijini Barcelona, Hispania akitokea katika mapumziko ya Christmas, waandishi wa habari wa Hispania walimfata Neymar na kumuuliza kama ni kweli Manchester City imekuwa ikimuhitaji na kujibu “Ndiyo ndiyo”.

Alipolizwa na waandishi wa habari kama kuna uwezekano wa yeye kuihama Barcelona na kuelekea klabu nyingine, Neymar alisema kuwa “kwa sasa siwezi kujua, maisha ni marefu lolote linaweza kutokea”



Hata hivyo kwa upande wa baba yake ambaye pia ndiyo meneja wa Neymar, Santos alinukuliwa mwezi uliopita akisema kwasasa wanafanya mazungumzo na Barcelona lakini bado kuna mambo hayajawa kama wanavyohitaji.

“Tunafanya mazungumzo na Barcelona lakini bado kuna mambo ambayo hayajawa sawa ambayo sisi tunayahitaji katika mkataba mpya,”alisema Santos.

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini