Mkutano wa huduma za hali ya hewa wafungwa Dar




Kutoka kushoto ni mwakilishi wa mradi wa CCIAM Prof. J.M. Abdallah, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi na Dk. Pascal F.Waniha.Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dk. Agnes Kijazi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi wa mradi wa CCIAM baada ya kufunga mkutano uliodumu kwa siku tano.Baadhi ya wawakilishi wa mradi wa CCIAM wakiwa katika mkutano huo.Baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka ya hali ya hewa nchini wakifuatilia mkutano huo.Mkutano ukiendelea.

TANZANIA imetoa wito kwa walimwengu kushirikiana katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani chini ya mpango wa kukabiliana na masuala hayo nchini (CCIAM) ili kutoa huduma bora kuhusiana na mabadiliko hasi ya hali ya hewa.

Hayo yalisemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Hali ya Hewa (TMA), Agnes Kijazi wakati akifunga mkutano kuhusu CCIAM ambao ni mpango unaohusisha taasisi nne nchini ambazo ni Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) na Idara ya Hali ya Hewa nchini (TMA).

Washiriki wengine ni taasisi kadhaa za nchini Norway zikiongozwa na Chuo Kikuu cha Sayansi za Maisha cha Norway (NMBU).

“Kwa vile mpango wa CCIAM unafikia mwisho, TMA imemua kufanya semina hii ili kushirikiana katika mafanikio ya kuendeleza nguvu za pamoja, ubunifu na ugunduzi kuhusiana na utoaji huduma unaohusiana na masuala ya hali ya hewa.

Kijazi alisisitiza kwamba mabadiliko makubwa ya hali ya hewa yametoa changamoto nyingi kwa nchi mbalimbali, ikiwemo Tanzania, ambapo athari zake katika sekta za kijamii na kiuchumi zinaonekana.

Alitokeza pia kwamba katika kuimarisha juhudi za CCIAM, idara yake imetoa mafunzo ya ngazi za juu kwa wafanyakazi wake ili kukabiliana na hali hiyo.

“Ujuzi uliopatikana, utaimarisha nguvu za TMA katika kutoa huduma bora zaidi na hivyo kuyafikia malengo ya miradi mbalimbali inayolenda kuleta usimamizi mzuri wa maliasili na mazingira kwa kupitia mbinu mbalimbali,” alisema.

P:ia aliishukuru serikali ya Norway kwa kutoa misaada ya fedha kwa mpango wa CCIAM na shughuli nyingine zinazohusika.

“Nazishukuru taasisi zilizoshirikiana nasi katika mpango huu na TMA itaendelea kushirikiana na vyuo vikuu mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha huduma bora zaidi zinazotolewa,” alimalizia kwa kusema.

NA DENIS MTIMA/GPL

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini