Serikali ya Magufuli yambana Zari

Zarinah Hassan ‘Zari’.

HAPA Kazi Tu! Serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli inazidi kuwanyoosha wakwepa kodi na sasa zamu ya utumbuaji majipu imemshukia Zarinah Hassan ‘Zari’ au mama Tifah, kwa kutaka asiandae tamasha kama lile la Zari All White Party lililofanyika mwaka jana kufuatia kukiuka baadhi ya masharti yanayoendana na ukusanyaji wa mapato ya serikali kupitia matamasha ya sanaa ya muziki.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mama Tiffah ametakiwa kutofanya shoo kama ile kutokana na ile ya mwaka jana iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City, Dar kuandaliwa kwa kukiuka baadhi ya masharti.

“Jamani kwa taarifa nilizozipata kutoka Basata (Baraza la Sanaa la Taifa), zinadai kuwa, Zari kwa sasa hataruhusiwa kuandaa tamasha hapa nchini hadi pale atakapofuata kanuni za Basata.

“Inasemekana Basata wamemuwekea ngumu baada ya kuandaa tamasha lake la mwanzo huku akishindwa kufuata baadhi ya taratibu zinazostahili kabla ya kuanza maandalizi.

“Kumbe mwaka jana (2014), Zari wakati anataka kuandaa shoo yake ya All White Party hakuzingatia sheria za Basata. Alianza kutangaza tamasha kabla ya kutoa taarifa kwao ili aweze kupewa kibali.

Ili kuisikia ishu hiyo kutoka Basata kwenyewe, juzi, Amani lilimpigia mmoja wa maafisa kutoka Basata ambapo alisema ni kweli Zari alikiuka baadhi ya taratibu ambapo alianza kutangaza shoo hiyo kabla ya kutoa taarifa Basata hivyo alipigwa fani ya shilingi laki tano (500,000).

“Kwa sasa sijui kama Zari anaweza kuruhusiwa kuandaa tamasha kwani kipindi kile anaandaa Zari All White Party alikiuka baadhi ya mambo likiwemo kuanza kutangaza shoo kabla ya kupata ruhusa kutoka Basata.

Rais Dk. John Pombe Magufuli.

“Mbali na hilo, pia kuna shilingi laki 5 ambazo alipigwa faini kufuatia kosa hilo hadi leo sina uhakika kama alilipa maana najua fedha aliyolipa ni milioni moja na nusu tu ambazo ni gharama za kulipia shoo,” alisema afisa huyo.

Ili kusikia kutoka kwa Zari, Amani lilimpigia simu mzazi mwenzake Zari, Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’ au baba Tiffah ambaye hakupokea na alipotumiwa meseji kwa simu ya mkononi, hakuijibu.

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini