Kane hauzwi kwa kiasi chochote – Pochettino




Kocha wa Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino (pichani) amesema timu yake haipo tayari kumuuza mshambuliaji wa klabu hiyo, Harry Kane kwa kiasi chochote ambacho kitawekwa mezani kwa ajili ya kupata saini ya mchezaji huyo.

Kane ambaye aliifungia Tottenham magoli mawili katika mchezo wa jumamosi dhidi ya Norwich amekuwa akionekana kuhitajika na baadhi vilabu ikiwemo Manchester United lakini Pottechino amesema mchezaji huyo hataondoka klabuni hapo na ataendelea kuitumikia kwa muda mrefu.

“Hakuna kiasi cha kumchukua, hakuna timu inaweza kumnunua … hayupo kwa ajili ya kuuzwa na hakujawa na thamani ya kumuuza sababu hatumuuzi,” alisema Pottechino.

Harry Kane kwa sasa amekuwa katika makali yake na tayari ameshaifungia magoli 11 kwa msimu huu na klabu yake inatarajiwa kucheza mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza leo saa 12 jioni dhidi ya Watford katika Uwanja wa Vicarage Road.


ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini