Ushindi wa Azam FC waishusha Yanga kileleni, cheki pichaz walivyoiadhibu Mtibwa Sugar Dec 30
Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena leo December 30 kwa mchezo mmoja wa kiporo kumaliziwa katika dimba la Azam Complex Mbande Chamazi. Huu ni mchezo ambao ulikuwa unakutanisha timu ambazo zinatafuta nafasi ya kusogelea kuelekea kileleni mwa msimamo wa Ligi.
Mchezo wa December 30 ulikuwa unazikutanisha timu ya Azam FC dhidi ya klabu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani. Huu ni mchezo uliokuwa umeteka hisia za watu wengi, kwani matokeo ya ushindi kwa Azam FC yalikuwa yanaishusha Yanga kileleni.
Katika dimba la Azam Complex licha ya klabu ya Mtibwa Sugar kuwa ugenini walifanikiwa kumiliki mchezo wa muda mwingi, lakini Azam FC walionekana kutulia na kucheza kwa mbinu kwa kiasi kikubwa. Mtibwa Sugar ambao nahodha wao Shabani Nditi aliingia akitokea becnhi baada ya kupona majeruhi. Walikubali kipigo cha goli 1-0.
Mtibwa Sugar walifanya makosa dakika ya 88 baada ya kumfanyia faulo nahodha wa Azam FC John Bocco nje kidogo ya eneo la hatari, hivyo Azam kupitia John Bocco wakapiga faulo hiyo na kupachika goli la ushindi na kufanya matokeo kumalizika kwa Azam FC kuibuka ushindi wa goli 1-0.
Kwa matokeo hayo Azam FC wanakuwa wanaongoza Ligi na kuishuka Yanga ambao walikuwa wamekaa kileleni kwa kuzidi michezo Azam FC. Yanga sasa wana jumla ya point 33 wakiwa wamecheza michezo 13, wakati Azam FC wana jumla ya point 35 wakiwa michezo sawa na Yanga.