Video-Wamekaa wanasubiri mwaka mpya, ghafla moto umezuka hotelini Dubai..


Wakati unahesabu dakika chache kuuvuka mwaka 2015 salama, najua kuna watu wangu wako kwenye nyumba za ibada wanamshukuru MUNGU, wengine wamekusanyika na ndugu jamaa na marafiki kwa utulivu kuenjoy huku wakisubiri na kuzihesabu kwa pamoja zile sekunde za mwisho za mwaka 2015 kwa amani kabisa, inanifikia taarifa kutoka Dubaikwamba jingo moja la Hoteli limewaka moto ghafla !!

Moto umeonekana kuwaka kwenye jengo la ghorofa lenye urefu wa mita 300 ambalo liko jirani na jengo refu la Dubai, Burj Khalifa huku watu wengi wakikusanyika kushuhudia tukio hilo.

Taarifa za mwanzo zimesema watu 16 ni majeruhi, vikosi vya zimamoto vimefanya kazi yao pia kuudhibiti japo chanzo cha moto hakijafahamika… Stori ninayo kwenye video hapa.


ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini