Mwanamke aliyezungushiwa duara jekundu ndiye anayedaiwa kumuua mumewe na kumfukia. NI simulizi ya kushangaza kufuatia Archard Frederick (41), kudaiwa kupigwa na kitu kizito kichwani hadi kufariki dunia na mkewe, chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi. Tukio hilo lilijiri Desemba 11, mwaka huu Kijiji cha Irogelo, Kitongoji cha Buhesi, Kamachumu, Muleba, Kagera. Akizungumza na gazeti mwenyekiti wa kijiji hicho, Prudence Rutaihwa alisema kabla ya Archard hajafariki dunia aligombana na mkewe. Alisema marehemu alipotea ghafla jioni ya Ijumaa ya Desemba 11, mwaka huu saa 12 jioni. “Jumamosi asubuhi wafanyakazi wenzake wa ujenzi walimpitia kwake ili waende kibaruani wakakuta mlango umefungwa. Walipompigia simu hakupatikana hewani, wakaondoka. Alisema wenzake hao walijua watoto walikwenda machungani na mkewe alikwenda shamba lakini baada kutopatikana hewani, kaka wa marehemu, Projest Fredrick alipewa taarifa na kuanza kuwa na wasiwasi. Kaburi alilozikwa ma...