Maiti yenye utata yafukuliwa na kukutwa imekatwa sehemu ya viungo na sehemu za siri


Hali ya taharuki imewapata wakazi wa kijiji cha Park Nyigoti kata ya ikoma wilaya ya Serengeti baada ya mahakama kutoa ruhusa ya kufukuliwa kwa mwili wa Bi. Celina Jumapili aliyefariki dunia na kuzikwa tarehe tatu Machi kisha kuonekana utata katika kaburi lake.

Kufuatia hali hiyo leo kaburi lake limefukuliwa na kukuta sehemu ya viungo vya  mwili wake vimekatwa  vikiwemo kiganja cha mguu vidole vya mkono wa kushoto na sehemu za siri zikiwa zimenyofolewa  hali iliyozua mashaka makubwa kwa wakazi wa  kijiji hicho.


Mwandishi wa habari hzi alifika katika kijiji cha Park Nyigoti wilayani Serengeti na kushuhudia zoezi la kufukua kaburi likiendelea ambapo inadaiwa kuwa marehemu Celina alifariki dunia tarehe mbili ya Machi na kuzikwa tarehe tatu lakini tarehe ishirini na mbili ndugu walikuta sehemu ndogo ya kaburi likiwa limefukuliwa.

Hali hiyo ndiyo ikawafanya wananchi wakataka kuhakiki kuwa mwili wa ndugu yao upo au umechukuliwa  na baada ya kupata kibali cha mahakama wamefukua na kukuta viungo hivyo vikiwa vimekatwa na watu wasio julikana.

Akielezea namna tukio ilo lilivyo tokea mama wa marehemu Celina Bi Nyahende Kwihamba amesema tukio hilo  limewaweka katika mashaka makubwa kutokana na kijiji hicho kushamiri kwa tabia ya ushirikina na kuiomba serikali isaidie kumaliza tabia hiyo.

Kijiji cha Park Nyigiti mara kwa mara kimekuwa na matukio ya kikatili kwani tarehe mbili ya mwezi marchi  watu watano waliuawa na wananchim kwa kuwatuhumu kuwa wanajihusisha na imani za kishirikina na tarehe saba ya mwezi wa pili kijiji jirani cha lubanda waliuawa watu wawili na kuchoma moto nyuma saba kwa kama tuhuma hizo hizo.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini