Kondom za MALAYA wa Morogoro zawaathiri watoto


Biashara ya ngono iliyokithiri katika mji wa Morogoro imegeuka kuwa kero kwa wakaazi wa eneo hilo na familia zao hali inayowaweka hatarini zaidi watoto wadogo wasio na hatia wanaokutana na kondom zilizotumika huku mkuu wa Mkoa huo, Mheshimiwa Joel Bendera akinawa mikono kuhusu suala hilo.
Wakati hayo yakiendelea Morogoro, serikali kuu imekuwa ikitafuta dawa kali ya kuweza kudhibiti biashara hiyo hapa nchini.
Edson Mkisi Jr wa Times Fm, hivi karibuni alitembelea mkoa huo na kushuhudia kushamili kwa biashara ya ngono sehemu mbalimbali za mkoa wa Morogoro hususani katika maeneo ya Kaumba na Itigi mkoani humo.
ndomu
Taarifa zilizopatikana awali toka kwa baadhi ya wakazi wa maeneo ya mji wa Morogoro zilidai kuwa biashara ya ngono imekuwa kero mkoani humo kutokana na utupwaji hovyo wa kondom zilizotumika katika mitaa hiyo.
Kondom hizo zilizotumika zinahatarisha afya ya watoto wanaozitumia kama mapulizo.
“Kiukweli hii biashara mbali ya kutuaibisha sisi akina mama lakini pia inatukera sana kutokana na utupwaji hovyo wa kondom unaofanywa na hao akina dada….na baada ya kondom hizo kutupwa watoto wetu wanaziokota na kuanza kupuliza kama maputo kwakweli inatukera sio siri,” anasema mama Sakina mfanyabiashara maarufu wa samaki Msamvu Morogoro.
Baadae mwendesha bodabodo eneo hilo alimuonysha mwandishi wetu Hotel moja maaufu na kudai kwamba Hotel hiyo imekodiwa na MALAYA  hao kwa ajili ya kufanyabiashara hiyo na serikali ya mkoa wanatambua ‘ishu’ hiyo!
ndomu
“Yaani hawa akina dada wakiwa ndani ya hiyo Hoteli hakuna mtu anayeweza kuwakamata ila wakifanya biashara yao nje ndio wanakamatwa na polisi kwa huku Morogoro maarufu kama Voda Fasta,” anasema dereva bodaboda huyo.
Kutokana na malalamiko mengi toka kwa wakazi wa Morogoro kuhusiana na uwepo wa MALAYA hao  katika viunga mbalimbali vya mkoa hao, Edson Mkisi Jr, mtangazaji wa kipindi cha Hatua Tatu cha times fm, aliamua kuwasiliana na Mkuu wa mkoa huo, Bw. Joel Bendara kwa ajili ya kujua serikali ya mkoa inafanya jitihada gani katika kupunguza ama kumaliza kabisa kero ya MAKAHABA  hao.
Mkuu huyo wa mkoa alidai kwamba hawezi kuzungumzia suala hilo la MAKAHABA wala utupwaji hovyo wa kondom kwa maelezo kwamba suala hilo lina hadhi ndogo sana ukilinganisha na cheo chake!
“Jamani hilo suala ni dogo sana kulingumzia mtu kama mkuu wa mkoa….naomba ufuate protoko mimi siwezi kuzungumzia kondom ukilinganisha na hadhi yangu hilo suala linamuhusu Mkuu wa Wilaya (DC), Meya ama Diwani sio mimi jamani,” alisema Bw. Bendera.
Alipoambiwa kwamba yeye ni kama rais wa mkoa na si vibaya kuweza kutoa neno kuhusiana na kero hiyo Mkuu huyo wa mkoa alisema; “Sasa hata kama ni rais wa mkoa ndio najua kila kitu? Kwa hiyo hata Kikwete anajua kila kitu kuhusu Morogoro? Ebu jaribu kuwa mtafiti kwanza hilo suala ni la level ya chini sana kuna watu sahihi wa kuweza kuzungumzia sio mimi…,” alisema Bendera.
Baada ya Mkuu huyo wa Morogoro ‘kumtolea mbavuni’ mwandishi wetu, mwenyekiti wa serikali za mitaa, mtaa wa Mwanzo Mgumu, Bw. Said Omari Kamba, mbali ya kukiri kukithiri kwa biashara hiyo, pia alikwenda mbali na kudai kwamba eneo la Itigi pia ni kichaka cha wauzaji na wanunuaji wa dawa za kulevya

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini