UKATILI KUBWA HUU: MASKINI MTOTO HUYU MDOGO AAJIRIWA NA KUTESWA NA MUAJIRI WAKE...!



Mbaya! Mtoto mwenye umri wa miaka (14) anadaiwa kuajiriwa akiwa na umri mdogo kinyume cha sheria za kazi kisha kupokea kipigo na manyanyaso kutoka kwa mtu anayedai ni bosi wake aliyemtaja kwa jina moja la Agness.


Mtoto mwenye umri wa miaka (14) ambaye ni mwenyeji wa Rombo mkoani Kilimanjaro anayeripoti manyanyaso kutoka kwa mtu anayedaiwa kuwa bosi wake. Kwa mujibu wa mashuhuda, mbali na kuwepo kwa malalamiko ya unynyasaji juu ya mtoto huyo, siku ya tukio mwajiri wake alimpa kipigo kwa madai kwamba alimuibia shilingi laki saba dukani alikomwajiri maeneo ya Mwananyamala, Dar hivi karibuni.
Mtoto huyo ambaye ni mwenyeji wa Rombo mkoani Kilimanjaro alizama jijini Dar na kuajiriwa katika duka hilo mwanzoni mwa mwezi Novemba, mwajka jana.

Akizungumza na mwanahabari wetu kwa masikitiko, mtoto huyo alisema tangu aajiriwe na mama huyo hajawahi kulala nyumbani bali alikuwa akilala hukohuko kwenye duka ambalo ni dogo halafu limejaa vitu vingi na alikuwa akifungua saa 12:00 asubuhi na kufunga saa 5:00 usiku kila siku.


Bosi wa mtuhumiwa, aliyefahamika kwa jina moja la Agness. Alidai kuwa hajawahi kulipwa mshahara ambao walikubaliana kwa malipo ya shilingi 25,000/= ambazo bosi huyo alitakiwa kuzituma kwa mama mzazi wa mtoto aliyeko Rombo.
Akielezea kwa uchungu mateso aliyoyapata tangu afike kwa mama huyo, mtoto alidai alikuwa akipigwa bila sababu na kusingiziwa kuwa ameiba fedha kisha kunyimwa chakula.

Kwa mujibu wa mtoto huyo, kuna mama mmoja jirani yao aliyekuwa akishuhudia mateso yake hivyo akawatafuta wanaharakati wa haki za binadamu ambao walichunguza ishu na wakajiridhisha kweli mtoto huyo alikuwa akinyanyaswa.

Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wanaharakati hao alisema kwa kuwa walishatoa elimu mitaani na kama yakitokea masuala kama hayo basi wananchi wawasiliane nao.

Mwanaharakati huyo alisema kuwa walipigiwa simu wiki mbili zilizopita kuwa kuna mtoto anateswa ndipo walipofanya uchunguzi katika eneo alilokuwa akifanyia kazi.
Wanaharakati hao waliwasiliana na polisi wa Kituo cha Oysterbay, Kinondoni, Dar ambapo mama huyo alikamatwa na kufunguliwa jalada la kesi namba OB/RB/5205/2014 UNYANYASAJI WA MTOTO huku akisubiri kufikishwa kwa kortini

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini