MAITI AZIKWA KIMAAJABU!


Mazishi ya Michael Krisantu yakiendelea
Na Waandishi Wetu
KATIKA hali isiyokuwa  ya kawaida na kushangaza, wananchi wa Mbezi Msakuzi Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, walisusa na kuondoka makaburini kwa kile kilichodaiwa kuwa maiti ya Michael Krisantu (pichani) waliyotarajia kuizika iliwekwa ndani ya  jeneza kimaajabu.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Makaburi ya Makamba Msakuzi, Mbezi jijini Dar es Salaam ambapo wananchi hao waligundua kuwa  maiti ya kijana huyo iliweka ndani ya jeneza kinyume na utaratibu uliozoeleka yaani kichwa chake kilielekezwa sehemu ya miguu na miguu ilielekezwa sehemu ya kichwa.
Msafara wa kuelekea makaburini kwa ajili ya mazishi ya Michael Krisantu.
Kama hiyo haitoshi, maiti hiyo badala ya kuviringishwa sanda nyeupe, ilitumika sanda nyeusi kitu  kilicholeta tafsiri tofauti miongoni mwa waombolezaji.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, kabla jeneza lenye mwili kutumbukizwa kwenye kaburi kulitokea mvutano mkubwa baina ya wanandugu na waombolezaji.
Waombolezaji wakizozana juu ya utaratibu wa mazishi ya Michael Krisantu.
Imeelezwa kuwa, waombolezaji hao waliwataka wanandugu wafuate taratibu zilizozoeleka katika jamii wakati wa kuzika.Hata hivyo, ndugu wa marehemu hawakuwasikiliza na kudai kwamba walikuwa wanafuata mila na tamaduni za kabila lao (jina la kabila linahifadhiwa kwa sababu maalum).
Mwili wa marehemu, Michael Krisantu ukishushwa kaburini.
Wanandugu hao wakaamua kushusha jeneza lenye mwili kaburini na walipoanza kuzika waombelezaji walikuja juu na kulitoa jeneza kaburini hali iliyosababisha kutokea kwa vurugu kubwa.
Wanandugu wa marehemu, Michael Krisantu wakiweka mishumaa pembezoni mwa kaburi la ndugu yao.
“Vurugu hizo zilisababisha wanawake waliokuwa makaburini kutimua mbio na wanaume wakasusa na kuwaacha wanandugu waendelee kumzika ndugu yao,” alisema shuhuda  wa tukio hilo kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini.
Marehemu Michael Krisantu enzi za uhai wake.
Habari zinasema kuwa, kutokana na utata huo, hata mchungaji aliyepaswa kuendesha ibada ya mazishi aliondoka bila kutoa huduma ya kiroho.
Mmoja wa wanandugu wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la Victor, alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo hakuweza kusema chochote badala yake alikuwa akibubujikwa na machozi.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini