CHADEMA WADAI KUENDELEA KUZUNGUMZIA KASORO ZA UANDIKISHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA PG4A2718

PG4A2718Chama cha demokrasia na Maendeleo chadema kimesema kuwa licha ya kuendelea kuwaelimisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, chama hicho pia hakitasita kuzungumzia changamoto zinazojitokeza wakati wa zoezi hilo

Kauli hiyo imetolewa na naibu katibu mkuu wa chama hicho Bara Mh. John Mnyika mara baada ya ufunguzi wa zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura lililofanyika kitaifa makambako mkoani Njombe

Mnyika amesema wanaipokeaa kwa mikono miwili kauli ya mwenyekiti wa Tume ya taifa ya uchaguzi kuwa vyama viwahamasishe wananchi kujiandikisha, na wao watazidi kufanya hivyo kwa kadri ya uwezo wao.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC) jaji mstaafu Damian Lubuva amesema teknolojia mpya ya kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura ni kwa ajili ya uandikishaji tu na halitatumika katika upigaji kura wala kuhesabu

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa uboreshaji wa daftari hilo la wapigakura mjini Makambako mkoani Njombe jaji Lubuva amewataka wadau mbalimbali kuhamasisha wananchi kushiriki kwa wingi katika zoezi hilo la kujiandikisha lililoanza jana

Amesema kwamba zoezi lililoanza mkoani Njombe limekwenda vizuri kwa lengo lililowekwa kuvukwa hali iliyoonesha kwamba zoezi hilo litafanikiwa vizuri.

WEKA MAONI YAKO HAPA

0 Maoni:

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini