Joyce Kiria Adaiwa Milioni 500 kama Fidia ya Kumdhalilisha Mbunge Kupitia Kipindi cha Wanawake Live

Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria amepokea samansi ya mashtaka kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir (CCM) ambaye amedai amlipe fidia ya kumdhalilisha sh. Milioni 500 au amuombe radhi kupitia  kipindi chake.

Akiongea na Mwandishi wetu, Joyce Kiria alisema kuwa amepokea barua hiyo kwa mikono miwili na anawasubiri wanasheria wake ili waijadili.“Nilimpokea mke wa Mbunge aitwaye Hawa kama mwanamke mwenye matatizo ambaye alifika kutoa sauti yake ili watu wamsaidie mtoto wake mwenye ulemavu.
 
"Baada ya kuongea naye nilimtafuta mheshimiwa ili kumpa nafasi naye aongee ya kwake kama wajibu wangu, lakini cha kushangaza yeye alinikamata na kunipeleka polisi, leo anasema nimemdhalilisha,” alisema Joyce .
 
Joyce anadaiwa fidia na Mbunge huyo kwa kuitangaza habari ya kumtelekeza mtoto mlemavu ambaye alipelekwa kwenye kipindi chake na mkewe, Hawa Deusi.   

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini