ELIMU YA MSAADA WA KISHERIA YAENDELEA KUWAOKOA WANANCHI WA KATA YA LUPILA MAKETE

 Na eddyblog, Makete
Wananchi wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kujitokeza kupatiwa msaada wa kisheria, na wasaidizi wa kisheria waliopo wilayani hapo ili kuwasaidia kutatua migogoro mbalimbali inayowakumba kutokana na ukosefu wa elimu ya sheria

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa chama cha wasaidizi wa kisheria wilayani Makete PACEMA ambaye pia ni msaidizi wa kisheria kata ya Lupila Bw. Nebert Sigala wakati akizungumza na mwandishi wetu kuhusu elimu ya masuala ya kisheria katika kata hiyo

Bw. Sigala amesema kwa hivi sasa wapo wananchi ambao wamekuwa wakijitokeza kupatiwa msaada wa kisheria ambao umekuwa ukiwasaidia katika matatizo yaliyokuwa yakiwakabili kwa kuwa hawakuwa na uelewa huo toka awali

Ametaja baadhi ya maeneo ambayo yamekuwa yakihitajika zaidi na wananchi hao kuwa ni sheria za ardhi, sheria ya mtoto pamoja na sheria mbalimbali za nchi, jambo ambalo limewasaidia wananchi wa kata hiyo kuona umuhimu wa kumiliki ardhi kisheria

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini