RADI YAUA MWALIMU NA WANAFUNZI 6 WAKIWA DARASANI


Kamanda wa Polisi Mkoani kigoma, Jafari Mohamed.
Wanafunzi sita, mwalimu wao, wamekufa papo hapo na wengine  11 kujeruhiwa kwa kupigwa na radi darasani wakati mvua kubwa zilizoambatana na kimbunga zikinyesha.

Tukio hilo lilitokea  saa 2:30 asubuhi katika Shule ya Msingi Nyakasanda iliyopo kijiji cha Nyaphenda wilaya ya Kasuru mkoani Kigoma wakati mwalimu huyo na wanafunzi hao wakiwa darasani. 
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, John Ndunguru, alisema kuwa tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita wakati mvua hizo zikinyesha.
Alisema mazishi ya mwalimu huyo na wanafunzi hao, yatafanyika leo mchana katika kijiji hicho chini ya usimamizi wa kamati ya ulinzi ya mkoa huo.
Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
 Hata hivyo Mohamed,  alisema majina ya waliokufa yatafahamika leo wakati wa mazishi yao.
Vilevile alisema wanafunzi wengine 10 na mwalimu wao waliojeruhiwa katika tukio hilo, wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa huo ya Maweni kwa matibabu.
Wakati huo huo; watu wanaoshukiwa kuwa majambazi, wamemuua kwa kumpiga kwa kitu chenye ncha kali Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Kigoma (Kiboa), Maneno Jackson.
Kamanda huyo  alisema kuwa mauaji hayo yalitokea usiku wa kuamkia jana baada ya majambazi hayo kuvamia nyumbani kwa Jackson eneo la Nazareti Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Alisema polisi wanaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha mauaji hayo.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini