Vurugu Ilula Mkoani Iringa, Mwananchi afariki, Kituo cha Polisi chachomwa moto!

 https://igcdn-photos-f-a.akamaihd.net/hphotos-ak-xaf1/t51.2885-15/10838341_940090139348117_466591223_n.jpg

WANANCHI wenye hasira mjini Ilula, mkoani Iringa, Jana wamevamia kituo cha polisi na kuvunja milango kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma moto baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili.


Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, tukio hilo limetokea jana asubuhi kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina lake kujigonga ukutani na kuanguka kisha kufariki dunia wakati akiwakimbia polisi waliokuwa kwenye oparesheni ya kuwakamata watu wanaokunywa pombe wakati wa asubuhi.


Habari zaidi zinapasha kwamba, licha ya kuchoma moto magari, waliziba barabara kuu ya kwenda mikoani na kuyazuia magari kupita, hali iliyosababisha polisi kuwakabili lakini walizidiwa nguvu na kuingia ndani ya basi la UPENDO.


Askari wakiwa ndani ya gari hilo waliendelea kushambuliwa na wananchi kwa mawe na kuvunja vioo vyake.


Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini