AMENIPA MIMBA ILA HANITAKI TENA, NIFANYEJE NAOMBENI MSAADA WA USHAURI ?

Mimi msichana mwenye umri wa miaka 24 nilikuwa na mchumba wangu ambaye tulikuwa tunapendana sana lakini baadae ikatokea ugomvi kati yetu tukawa hatuelewani, 

kumbe kipind tunagombana tayari mimi nilikuwa mjamzito bila kujijua. Nilipojigundua kuwa ni mjamzito nikamtafuta kwenye simu hakupokea, nikamtumia sms hakujibu, ikabidi nimtafute kaka yake, ndio akatukutanisha. 
Lakini cha ajabu huyu kaka alikataa mimba. Sikukata tamaa ya kumtafuta na kumsihi ili akubali tulee mimba lakini msimamo wake ulikuwa palepale na mpaka sasa mimba inaelekea miezi mitatu..Juzi nimemtumia sms akanijibu na chakushangaza alinambia hivi "huyo mtoto hata akizaliwa asinijue na pia atakuwa na laana tupu na usije hata siku moja ukamwambia mi ndio baba yake"...
Nina mawazo sana ndgu zangu, nifanyeje, niache kumtafuta kwenye simu na niendelee kulea mimba, niitoe au nisichoke kumtafuta? Ila ananitukana jamani hana hata huruma tena matusi makubwa sana...naomben ushauri wenu!!

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini