CHENI YA SHILINGI MILILIONI 6 YAMFIKISHA POLISI AUNTY EZEKIEL


Nyota wa sinema Bongo, Aunty Ezekiel akiwa Bongo.
Stori: Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani NYOTA wa sinema Bongo, Aunty Ezekiel ameingia matatani na maafande wa Kituo cha Polisi Pangani, Ilala jijini Dar akidaiwa kutokomea na cheni ya Shabani Limo yenye thamani ya shilingi milioni 6.

 Kwa mujibu wa chanzo, mwishoni mwa Februari, mwaka huu, Aunty alikwenda kwa Shabani na kuazima cheni hiyo kwa makubaliano ya kuirejesha baada ya muda jambo ambalo hakulifanya na baadaye, Septemba mwaka huu, akasafiri kwenda Marekani kutangaza utalii wa ndani.
 Baada ya kurejea, Oktoba mwaka huu, Shabani alimkomalia Aunty na kufikishana Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar ambapo staa huyo alisema na yeye alimwazima cheni hiyo rafiki yake aitwaye Neema.
 Ilidaiwa kuwa, Neema baada ya kubanwa alikiri na kusema aliiweka bondi cheni hiyo na hapo ndipo danadana zilipoanza hivyo jamaa akaamua kwenda kufungua madai mengine Kituo cha Polisi Pangani.
 Jumatano iliyopita, mapaparazi wetu walifunga safari mpaka kituoni hapo ambapo baadhi ya askari walikiri kuwepo kwa kesi hiyo lakini waligoma kutoa namba za kumbukumbu za jalada ‘RB’ wakidai mwenye uwezo huo ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova.




Aunty Ezekiel akiwa Marekani alipokwenda kutangaza utalii wa ndani.
 “Ni kweli hapa kuna hiyo kesi na ilianzia Oysterbay japo hatuwezi kuitolea maelezo ya kina kwa vile jambo lenyewe limekaa kimapenzi zaidi,” alisema askari mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.
Shabani alipotafutwa kwa njia ya simu na kuulizwa juu ya taarifa hizo alisema alimuazima Aunty cheni hiyo ambapo naye alimpa shoga yake.

 Aunty alipopatikana na kuulizwa alikana kumfahamu Shabani na kudai hana taarifa zozote za kuwepo kwa ishu hiyo.“Mh! Huo ni uzushi, hakuna kitu kama hicho na wala hizo taarifa sizifahamu, huyo mwanaume simjui ndiyo kwanza namsikia kwako,”alisema Aunty.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini