KALI YA MWAKA!!!WAFUMWA LIVE CHUMBANI, KIDUME AKIMBILIA DARINI! CHEKI PICHA
Mbaba
Kibole Kalepe akiwa darini kuepusha kipigo baada ya fumanizi. Tukio
hilo lililofunga umati wa watu wapenda ubuyu lilijiri Oktoba 28, mwaka
huumaeneo ya Iteba-Sinza, jijini Dar baada ya mwenye mali, aitwaye
Fikiri kurejea ghafla nyumbani na kumkuta mkewe akiwa chumbani na Kibole
wakifanya yao.HILI ni fumanizi la aina yake! Achana na mafumanizi ya
kawaida ambayo yamezoeleka, la safari hii ni la kipekee baada ya mgoni
aitwaye Kibole Kalepe kukutwa chumbani na mke wa mtu, Asha Hemedi
(pichani) kisha kukurupuka na kupanda darini haraka kukwepa kipigo,
Ijumaa lina mkasa kamili.
Mke wa mtu, Asha Hemedi akihamaki baada ya fumanizi.
SIKU YA TUKIO
Kwa mujibu wa
chanzo makini, siku ya tukio Fikiri ambaye ni dereva wa masafa marefu
aliaga kwamba anasafiri lakini akiwa hajafika mbali, gari liliharibika
na kurudi nyumbani kuchukua vifaa na kabla hajagonga mlango, alisikia
sauti ya mkewe na Kibole.
Mke wa mtu, Asha Hemedi akitaitiwa eneo la tukio. UVUMILIVU WAMSHINDA
Chanzo hicho
kilizidi kushusha mistari kwamba, baada ya kusikia sauti hizo, Fikiri
hakuweza kuvumilia aliamua kuwakatisha kwa kuwagongea mlango huku
akitaja jina la mkewe ili amfungulie lakini hata hivyo ilichukua muda
mrefu mlango kufunguliwa.
Makamanda wa Polisi wakimsindikiza Kibole Kalepe kwenye gari kuelekea kituo cha Polisi Magomeni. MLANGO WAFUNGULIWA
“Mume aliendelea kugonga mlango, baada ya muda mrefu kupita ukafunguliwa ambapo mke alikutwa akiwa ameloa jasho na kuhema kwa kasi kutokana na hofu, hata hivyo alikua amefunga khanga moja tu.
Mke wa mtu Bi. Asha Hemedi naye akichukuliwa na Polisi kuelekea kituoni.MGONI JUU YA DARI
“Mume alipoangalia kila kona kumtafuta mwanaume aliyekua naye hakumuona na alipochungulia darini alimuona mgoni wake amejificha, baadaye aliomba wapigiwe simu polisi waje kumuokoa,” kilisema chanzo.
Mtuhumiwa Kibole Kalepe na mke wa mtu wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi. ACHIMBWA MKWARA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kwamba, wananchi wapenda mambo ya watu waliokuwa
wamezingira nyumba hiyo walimwambia yeye ni mwizi hivyo watamshushia
kipondo hevi, mgoni huyo alikataa na kudai kwamba hakuwa mwizi bali
mgoni hivyo wasimuue.
“Jamani mimi siyo mwizi mimi ni mgoni, niitieni polisi,” alisikika Kibole.
Raia wakiwazodoa wagoni wakati wakipelekwa Kituo cha Polisi Magomeni. POLISI WAMTAITI
Wananchi walimuelewa
wakaita polisi ambapo ndani ya muda mfupi walifika na kumshusha darini
kisha kumkamata na mwananke wakawapeleka Kituo cha Polisi Magomen