Ndoa ya Shilole na Mchumba Wake Nuhu Mziwanda Haipo Tena
IMEGUNDULIKA
kuwa uhusiano wa staa wa Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, na mpenziwe
Nuh Mziwanda ni kazi bure kwani uwezekano wa kufunga ndoa kati yao haupo
kutokana na kupishana imani.Ishu hiyo imejidhihirisha juzikati nyumbani
kwa wawili hao Mwananyamala-Manjunju jijini Dar, baada ya paparazi wetu
kuwaibukia na kutaka kujua malengo yao zaidi kama wana mpango wa kuoana
au la, msikie kwanza Nuh:
“Mimi
ninampenda Shilole kwa asilimia 100, ila siko tayari kubadili dini kwa
ajili yake maana kwetu ni wakristo na hapa naongea mama yangu ni mzee
wa kanisa hivyo Shilole naamini anaweza kubadili maana mimi tayari
nimeshafanya mengi sana juu yake.”
Msikie Shilole: Mimi siwezi kubadili dini maana Nuh ndiye alisema atabadili hata hivyo familia yangu haiwezi kunikubalia kubadili dini kwa ajili ya kufunga ndoa kama amesema naye hawezi kubadili basi tutaishi tu maana hata ndoa ya serikali yenyewe hawezi na maisha siyo lazima tuoane.”