MWANAMKE LULU WA Y-TONE NAYE AINGIA KWENYE AIBU KWA KUPIGA PICHA MBAYA
Wauza nyago wanaotumika katika video mbalimbali za wasanii wa Bongo Fleva (video queens) wametia fora kwa kurekodiwa mikanda ya utupu na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na simu za kupangusa.
Ukiachana
na Agness Gerald ‘Masogange’, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack
Patrick’, Rehema Fabian, Husna Maulid ambao walisharipotiwa huko nyuma,
mrembo maarufu kwa jina moja la Lulu ambaye ameuza sura kwenye ‘kioo’
cha Ngoma ya Shitobe ya msanii anayefahamika kwa jina la Y-Tony, naye
ameingia katika skendo hiyo.
Uchunguzi
wetu ulibaini kwamba, asilimia kubwa ya warembo hao hurekodiwa na
wapenzi wao wanapokuwa faragha kunako sita kwa sita na pale
wanapogombana ndipo wanaume hao huzitupia video hizo mitandaoni ili
kuwakomoa na kuthibitisha kuwa tayari amempitia hivyo ni ‘makapi’.
Kupitia
Mtandao wa Youtube, mrembo huyo anaonekana kwenye video akicheza muziki
wa Bendi ya Yamoto, akiwa mtupu huku ikisikika sauti ya mwanaume
ikimsihi aendelee kucheza kwa ahadi kuwa video hiyo ni maalum kwa ajili
yake na si mtu mwingine.
“Hii ni special for me, not for anyone,” alisikika mwanaume huyo.
Video
hiyo ambayo ilisambaa haraka mwanzoni mwa wiki hii na kuwa gumzo katika
mitandao mbalimbali, wafuasi wengi walikuwa wakikemea tabia hiyo ya
kurekodiwa wakiwa utupu.
“Hawa
wanajitakia wenyewe, haiwezekani uwe na mpenzi halafu umuamini eti
akurekodi kwa ajili yake tu, ni ujinga tu unawasumbua. Kwanza unaruhusu
kurekodiwa ili iweje?,” alihoji mdau mmoja mtandaoni.
Baada
ya kuitia kibindoni video hiyo, mwandishi alimsaka Lulu wa Video ya
Shitobe (siyo Elizabeth Michael) kupitia rafiki zake lakini jitihada
ziligonga mwamba kwani ilidaiwa kwamba, kutokana na aibu aliyoipata,
aliamua kujificha huku akizima simu sambamba na kufuta picha zote kwenye
akaunti yake ya Instagram.
Licha
ya kuzifuta, mwanahabari wetu alibahatika kumpata kupitia Facebook
ambapo anatumia jina la Lulu Mrs Comoro ambako ametupia picha zake
lakini akashindwa kutoa ushirikiano.
Mtiririko
wa warembo hao kurekodiwa video za ngono ulianza kwa Rehema ambaye
alionekana kwenye video ya msanii wa Bongo Fleva aitwaye Pasha.
Baadaye
Agness ambaye alishiriki kwenye video ya Wimbo wa Masogange wa Belle 9
akafuata Jack Patrick ambaye ameshiriki kwenye video ya Chungwa ya
msanii Sumalee na Nataka Kulewa ya Diamond akafunga dimba kabla Lulu
hajaongeza idadi hiyo.