Hii inahusu uzinduzi wa ujenzi kiwanja kingine cha michezo Dar es Salaam.


Rais Kikwete akihutubia wakati wa uzinduzi wa ujenzi huo.

Rais wa Jakaya Kikwete leo amezindua ujenzi wa kituo cha Michezo katika eneo la Kidongo Chekundu, Mnazi Mmoja Dar es Salaam.
Kituo hicho kinajengwa kwa ufadhili wa klabu ya Sunderland ya Uingereza, ambapo baada ya kukamilika kitakuwa kinatumika na umma katika michezo mbalimbali.
Katika uzinduzi huo Rais ameagiza uongozi wa TFF uisimamie kila timu inayoshiriki ligi kuu iwe na timu ndogo ili kuandaa wachezaji wa baadaye, huku akiagiza shirikisho hilo kubeba jukumu la kumlipa kocha wa taifa badala ya kuitegemea Serikali.
Baada ya kukamilika kwa ujenzi huo, Sunderland imeahidi kutoa msaada wa wataalamu wa michezo wa mpira wa miguu ili kusaidia kuboresha viwango vya wanamichezo.




Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini