MSIBA WAMSOTESHA AISHA MADINDA DUBAI

Stori: Gladness Mallya
ZOEZI alilokuwa akilifanya Mkurugenzi wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka la kufanya mpango wa kumrudisha nchini mnenguaji Aisha Madinda amelisitisha kwa muda baada ya kupata msiba mzito wa mdogo wake na kumfanya mwanadada huyo aendelee kusota Dubai.Akizungumza na gazeti hili, Asha alisema alipata msiba wa mdogo wake anayemfuata aliyekuwa akiishi nchini Ubelgiji hivyo hajawasiliana na watu waliokuwa wakilishughulikia suala la Aisha pia bado fedha zinazohitajika hazijapatikana.
“Sijajua kinachoendelea kwani baada ya kupata msiba sijawasiliana na wale watu wa Dubai tena hivyo kuanzia wiki ijayo (wiki hii) nitaanza kulifuatilia suala hilo tena kwani fedha zilizokuwa zinatakiwa awali ni dola 800 na bado hazijapatikana na hivi alivyoendelea kukaa zitakuwa zimeshazidi zaidi ya hizo,” alisema Asha.Aisha Madinda aliondoka nchini baada ya kupata shavu la kwenda kucheza shoo Dubai lakini baada ya kufika huko, wenyeji wake walimgeuzia kibao na kumnyang’anya pasipoti yake kisha kumtumikisha kazi za ndani.
Wakati gazeti hili linaenda mtamboni, taarifa zilizotufikia zilikuwa zikieleza kwamba Aisha ameshawasili nchini baada ya kusaidiwa na ubalozi wa Tanzania huko Dubai.
CREDIT: GPL

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini