RAIS NKURUNZIZA AWAFUTA BAADHI YA VIGOGO KWENYE NYADHIFA ZAO
Na RFI
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amewafuta washirika wake wa karibu kwenye nyadhifa zao.
Mkurugenzi kwenye afisi ya rais jenerali
Alain-Guillaume Bunyoni na mkuu wa Idara ya Ujasusi jenerali Adolphe
Nshimirimana ambao wamekua na ushawishi mkubwa kwenye utawala wa Pierre
Nkurunziza, wameondolewa kwenye nyadhifa zao.
Si hao tu, maafisa wengine waandamizi
wamefutwa kwenye nyadhifa zao, ikiwa ni pamoja na wakurugenzi wawili
kwenye afisi ya rais. Maafisa hao waandamizi wanadaiwa kuwa miongoni mwa
vigogo wenye ushawishi mkubwa kwenye utawala.(P.T)
Uamzi huu ambao umewashangaza wengi,
umetolewa baada ya kufanyika vikao vya siri. Hakuna mtu ambaye
angelifikiri kuwa hali hii ingelitokea. Jenerali Alain Guillaume
Bunyoni, ambaye ni miongoni mwa vigogo hao katika utawala wa Cndd-Fdd
amekabidhi madaraka leo Ijumaa asubuhi, na nafasi yake imechukuliwa na
raia wa kawaida. Kwa sasa Bunyoni ni katibu mtendaji wa Baraza la
usalama wa taifa. amekua kama amewekwa kapuni.
Jenerali Adolphe Nshimirimana mkuu wa
Idara ya Ujasusi, ambaye aliwahi kua mkuu wa majeshi wakati walipokua
bado msituni na ambaye amekua akiendesha ukaguzi katika sekta nzima ya
usalama, ameondolewa kwenye wadhifa wake, nafasi hiyo imechukuliwa na
mkuu wa zamani wa majeshi, jenerali Godfroid Niyombare.
Maafisa wengine waandamizi ambao wana
ushawishi mkubwa kwenye utawalawa Cndd-Fdd wamefutwa kwenye nyadhifa
zao. Hali hii inatokea baada ya hali ya sintofahamu kuripotiwa katika
uongozi wa juu wa maafisa wa kijeshi kutoka waasi wa zamani wa Cndd-Fdd.
hata hivo, inaarifiwa kuwa sakata hilo bado linaendela.