HAWA MA HOUSEGIRL: APEWE PIGO NA KUFUKUZWA KAZI

Na Victor wa Bongo SpeciaL
Nimeskia kilio cha ajabu kama vile ubaya umefanyika kwa mtoto wa jirani yangu. Baada ya muda, mmoja wapo ya house girl aliingia nyumbani kwangu akiomba kwa kutetemeka nije kuwasaidia.
Nilipo fika, nilikuta mtoto amechanika kwanzia puani hadi mdomoni na damu kumwagika sana sana. Mama wa mtoto hayupo nchini Na mumewe kazini,

MSAADA WANGU
nilipeleka mtoto hospitali hapo hapo, Mtoto alishonwa.



MAAMUZI YA BABA WA MTOTO
Alimpiga house girl na kumwachisha kazi hapo hapo, akamlipia basi moja kwa moja ili aweze kurudi kwao. Akamnyima hela yake yote ya mshahara akidai kuwa ni hela ya matibabu ya mwanaye aliyempiga.



Watu hawajafurahia mamuzi ya huyu mzazi ambaye angechukuwa huyu house girl  hatua na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria. Apewa adhabu inao stahili. Tuta kumbuka house girl wa Uganda na huyu wa hapa hapa kibaha aliemua mtoto wa miaka mitatu. Tusikae kimya na kuacha hayo mabaya kuendelea mtaani kwetu. Vile vile hawa house girl ni watoto, ni wadada ni wa mama wa watu. Kuwa nyanyasa sio dili. Kumbuka mama kwa kiwango kikubwa na baba kwa kiwango kidogo kwamba unapo mnyanyasa utaenda kazini na mwanao atapewa kipigo kwa ulichomfanyia


Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini