AUNTY LULU ASIMULIA ALIVYOBAKWA


Mwanadada mwenye taito ya utangazaji na uigizaji wa sinema za Kibongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ amefungua kinywa na kutoa la moyoni akisimulia tukio baya lililowahi kumkuta la jinsi alivyobakwa.
 
Akizungumza na Gpl, Aunty Lulu asiyeishiwa na vimbwanga alisema kwamba, kamwe hawezi kusahau tukio hilo maishani mwake.

Aunty Lulu aliyeng’ara kwenye Sinema ya Lost Soul alieleza namna alivyobakwa na rafiki wa shemeji yake (rafiki wa mume wa dada yake) na kumpotezea ndoto zake za kuanza mchezo huo akiwa ndani ya ndoa.
 
Akieleza kwa uchungu na masikitiko, Aunty Lulu alitiririka kwamba, alikuwa akiishi kwa dada yake ambapo rafiki wa mume wa dada yake huyo alikuwa na mazoea ya kufika nyumbani kila wakati alipokuwa akifanya kazi maeneo ya Posta jijini Dar.

Aunt Lulu alisema kwamba wakati huo, yeye alikuwa akisoma Shule ya Sekondari ya Kisutu, Dar, hivyo kila siku jioni mwanaume huyo alikuwa akimpitia na kumpa lifti hadi nyumbani.
 
Aliendelea kusema kwamba, siku moja jamaa huyo aliyekuwa amemzidi umri maradufu alimtaka wafanye mapenzi lakini alimkatalia kwa madai kwamba hakuwahi kufanya mchezo huo mbaya ambao alifundishwa kuwa ni dhambi.

“Kwa kawaida yule jamaa alikuwa akinifikisha nyumbani kwa dada yangu pale Makumbusho (Dar), ananisubiri, nabadilisha nguo, naenda naye kwake maeneo ya Block 41 (Kinondoni) ambako alikuwa akinifundisha. So alinibakia nyumbani kwake,” alisema Aunty Lulu, mtangazaji wa zamani wa ITV na C2C.

Staa huyo aliendelea kutiririka kwamba alipomwambia kuwa hajawahi kufanya kitendo hicho, mwanaume huyo alimwambia haamini ndipo akamkamata kinguvu na kumpeleka chumbani kwake kisha akamwingilia na kumsababishia maumivu makali. 
 
“Kwa kuwa niliumia sana, nilikuwa natembea kwa shida hivyo dada yangu aligundua.

“Ilibidi dada anibane kujua nina tatizo gani. Kwa kuwa nilikuwa sina ujanja nilimwambia nimeingiliwa kwa mara ya kwanza lakini nilisita kumtaja mwanaume huyo.
 
“Dada aliponibana sana nilimwambia kwamba niliingiliwa na huyo rafiki wa mume wake.

“Lilikuwa ni tukio la kusikitisha sana na ukweli liliwaumiza sana dada na shemeji yangu.
 
“Walimsema sana mwanaume huyo na ikawa ndiyo mwisho wa urafiki wao.

“Umri sikumbuki lakini nakumbuka nilikuwa nakaribia kuingia kidato cha nne. Yule mwanaume alizoea kuninunulia vifaa vya shule na kunisisitiza kusoma.
 
“Nilimuona mtu bora sana, nikamzoea na ikawa rahisi kwenda kwake kusoma maana jamaa alikuwa ‘jiniazi’ na mwanzoni alikuwa jirani yetu kabla ya kuhama.
 
“Ukweli huwa sipendi kuelezea historia ya maisha yangu ya mapenzi kwani inaniumiza sana.

“Huwa najisikia kulia kwa sababu huyo rafiki wa shemeji yangu alinipotezea ndoto nilizokuwa nazo kwamba nitafanya juu chini niolewe nikiwa ‘mbichi’ hivyo mapenzi ningefanya nikiwa ndani ya ndoa.
 
“Sikufurahia kabisa kitendo hicho maana naona pia kiliniathiri kisaikolojia,” alisema Aunty Lulu.

“Baada ya tukio lile aliomba anioe ili nimsamehe lakini nilikataa. Baadaye alikwenda kusoma nje ndipo tukapotezana na sijawahi kumuona tena, nasimulia ili liwe fundisho kwa wanawake wanaopenda kuwa na ukaribu kupitiliza na wanaume wasiowajua kiundani,” aliweka nukta Aunty Lulu.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini